HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 20, 2026

TOP ARCHIVE YAJIVUNIA CHETI CHA KIMATAIFA CHA ISO 22301

KAMPUNI ya Top Archive imesema kampuni hiyo kupata cheti cha kimataifa cha ISO 22301:2019 cha Mfumo wa Usimamizi wa Uendelevu wa Biashara (BCMS) ni hatua kubwa inayoonesha uimara na utayari wao katika kukabiliana na changamoto za kiutendaji.Akizungumza leo Aprili 20,2026 Mkurugenzi Mtendaji wa Top Archive,Paul Muhato ameeleza  cheti hicho ni uthibitisho ambao unaakisi dhamira ya kampuni katika kuhakikisha inaweka mifumo madhubuti ya kuendeleza shughuli zake hata pale kunapotokea majanga au misukosuko isiyotabirika.


Amesisitiza kwamba “Cheti hiki si tu utambuzi wa kawaida, ni ishara ya kujitolea kwetu kuhakikisha tunatoa huduma bora kwa wateja wetu bila kukatizwa, hata katika mazingira magumu.

“Mafanikio haya yametokana na ushirikiano, nidhamu, na juhudi za pamoja za wafanyakazi wa kampuni yetu ambao wamekuwa mstari wa kuhakikisha tunafuata viwango vya kimataifa.”

Akifafanua zaidi amesema cheti hicho kinatoa uhakika na kuimarisha imani kwa kuwa kinaonesha kuwa Top Archive ni kampuni ambayo inayozingatia usalama wa taarifa, usimamizi wa hatari, na ulinzi wa maslahi ya wateja wake.


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad