
Mratibu Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akiangalia moja ya matrekta yanayotumiwa na walimu wa Shule ya Sekondari Msangano kwa kufundishia wanafunzi amali kwa vitendo mkoani Songwe, wilaya ya Momba.

Mratibu Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akimpongeza mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msangano baada ya kutoa burudani kwenye hafla ya ziara ya wadau wa elimu wanaoshiriki maadhimisho ya GAWE 2026 walipotembelea shule hiyo.

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msangano wakitoa burudani kwenye hafla ya ziara ya wadau wa elimu wanaoshiriki maadhimisho ya GAWE 2026 walipotembelea shule hiyo.

Wadau wa elimu wanaoshiriki GAWE 2026 wakiwa ziarani.

Mratibu Taifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), Bi. Martha Makala akiangalia moja ya matrekta yanayotumiwa na walimu Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Msangano wanaochukua mafunzo ya amali kwa vitendo mkoani Songwe, wilaya ya Momba.

Ziara katika Shule ya Sekondari Msangano inayotoa amali kwa vitendo mkoani Songwe, wilaya ya Momba.

Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wakitembelea Shule ya Sekondari Msangano na kujionea wazi namna elimu ya amali inavyotekelezwa kwa vitendo mkoani Songwe, wilaya ya Momba.
.jpg)
Wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) na wadau wa elimu wakitembelea Shule ya Sekondari Msangano na kujionea wazi namna elimu ya amali inavyotekelezwa kwa vitendo mkoani Songwe, wilaya ya Momba.
WANACHAMA wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) pamoja na wadau wa elimu wanaoshiriki maadhimisho ya Juma la Elimu Kitaifa wamefanya ziara katika Shule ya Sekondari Msangano na kujionea wazi namna elimu ya amali inavyotekelezwa kwa vitendo mkoani Songwe, wilaya ya Momba.
Shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi wa mkondo wa amali 155 tangu kuanzishwa kwake mwaka 2024, licha ya kuwa na changamoto kama ukosefu wa vifaa vya kujifunzia kwa vitendo kwa fani ya Afya ya Wanyama, walimu wa amali na karakana, wanafunzi wameonesha muitikio, uelewa mkubwa, na furaha yao katika kujifunza masomo ya amali.
Kwa upande wake Rahabu (15), mwanafunzi wa kidato cha tatu ambaye alionesha umahiri wake katika kuendesha trekta amewataka Watoto wakike nchini kote kujiamini na kuona kwamba wanaweza. “Mabinti wapambane, wasikate tamaa. Mara nyingi hofu ndio huwa changamoto kubwa kwa mabinti, mimi nawashauri waache uogo kwakua hakuna mtu atakaye wang’ata wala kuwacheka, ujasiri ni kitu muhimu sana kwa msichana ili aweze kutimiza ndoto zake”, amesema Rahabu.
Awali akizungumza katika ziara hiyo, Mratibu Taifa wa TEN/MET, Bi. Martha Makala, amepongeza juhudi za serikali katika kuendeleza elimu nchini, hususan katika kuimarisha elimu ya amali ambayo imeonekana kuwa nyenzo muhimu ya kuwajengea wanafunzi ujuzi wa kujitegemea na kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi.
Aidha, ameiomba Srerikali kutenga bajeti ya 2026/27 ili kujenga karakana itakayo ongeza ufanisi katika utekelezaji wa masomo ya amali pamoja na walimu wa amali na dereva katika shule hiyo ili kusaidia ujifunzaji wa matumizi ya vyombo vya amali.
Wadau hao wa elimu wakiwa wilayani Momba, pia walitembelea Shule ya Msingi Elimu Maalumu na kituo cha IPOSA Ndalambo iliyoanzishwa mwaka 1959, na kushuhudia mafanikio makubwa katika kurejesha matumaini kwa vijana waliokua wamekata tamaa kwa kuwapa fursa ya kupata ujuzi kupitia IPOSA, upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wote, uwepo wa bustani ya mboga mboga na kitalu cha bustani ya miti.
Kupitia kituo hicho cha elimu changamani vijana walioko nje ya shule, wanajifunza fani kama ushoni, uselemala, uashi,uchomeleaji, upishi na elimu ya ujasiriamali. Shule ya Ndalambo pia ina jumla ya wanafunzi 52 wa elimu maalumu/jumuishi.
Akizungumzumza na ugeni wa TEN/MET, Mhe Diwani, Samuel Kilanga ameeleza kuwa licha ya juhudi za serikali na wadau kuwezesha shule hiyo, shule inakabiliwa na changamoto zikiwemo upungufu wa madarasa, vyoo, walimu wa elimu maalumu na miundombinu mingine muhimu, huku akiomba wadau waendelee kuwekeza ili kutatua changamoto hizi.
Naye mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, alibainisha mafanikio ikiwa ni pamoja na, kurejesha wanafunzi waliokatisha masomo hususan mabinti, pamoja na kuongeza mwamko wa jamii kuchangia elimu ambapo kwa miaka minne wamekua wakijenga madarasa ambayo yanahitaji nguvu Zaidi ili kukamika.

No comments:
Post a Comment