Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa tuzo kwa washindi 10 wa shindano la insha la viwango la mwaka 2024/2025, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika mwaka 2026.
Washindi hao wametoka katika vyuo mbalimbali nchini, ambapo jumla ya washiriki walikuwa wanafunzi 522 wa elimu ya juu kati yao, wanawake walikuwa 230 na wanaume 292, huku shindano hilo likiratibiwa na Shirika la Viwango Afrika (ARSO).
Akizungumza leo Aprili 9, 2026 jijini Dar es Salaam katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria wa TBS, Dkt. Candida Shirima, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, amesema taasisi hiyo inatambua mchango wa washiriki hao katika kuongeza uelewa wa viwango na kuelimisha jamii.
Amesema viwango vina mchango mkubwa katika kukuza biashara kwa kuongeza uaminifu kwa walaji, kuchochea biashara endelevu na kukuza uchumi wa taifa, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia viwango kila siku.
Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa shindano hilo, Dkt. Jalia Muna, amesema insha tano bora kutoka kwa washindi hao zitawasilishwa ARSO kwa ajili ya kushindanishwa barani Afrika, na maoni ya washindi yatasaidia kuboresha utendaji kazi wa TBS.

No comments:
Post a Comment