HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 17, 2026

RAIS SAMIA ATUNUKIWA TUZO YA KIMATAIFA YA UBINADAMU , UPASUAJI WA UBONGO

 

(HUMANITARIAN AWARD)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo maalum ya  kimataifa ya Ubinadam ya upasuaji wa ubongo, kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha sekta ya afya nchini. 

Tuzo hiyo imetolewa leo Aprili 16,2026 na Rais wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo Mgongo na mishipa ya fahamu Tanzania Dkt. Othman W. Kiloloma katika mkutano wa pili  wa kimataifa wa Shirikisho la Jumuiya ya Upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu.

"Kwa niaba ya Chama cha Wataalam wa upasuaji wa ubongo na mgongo tunakutambua na kukushukuru kwa mchango wako mkubwa wa ubinadamu, ni heshima yangu kubwa kukukabidhi tuzo ya ubinadamu ya upasuaji wa ubongo, hongera sana"

Dkt. Kiloloma amesema katika taaluma ya upasuaji wa ubongo, muda ni uhai na mifumo madhubuti ndiyo huamua hatima ya mgonjwa, kupitia uongozi wako thabiti Tanzania imeimarisha uwezo wa kukabiliana na magonjwa hatarishi ya ubongo na uti wa mgongo.

Amesema kuwa, kupitia uwekezaji uliowekwa na Serikali ya awamu ya sita katika huduma za kibingwa na ubingwa bobezi, ujenzi wa rasilimali watu na uimarishaji wa huduma za vipimo, dharura na bima ya afya kwa wote umeokoa maisha na matumaini ya maisha ambayo wengine hawakuwa nayo.

"Tuzo hii haitambui sera pekee, bali utekelezaji na matokeo yameonesha kuwa, uongozi wa kweli unaweka utu wa binadamu katikati ya maendeleo ya taifa" amesema Dkt. Kiloloma


 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad