
Na John Mapepele, New York -Marekani
Waziri wa Afya Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa ameongoza timu ya Tanzaniani katika Mkutano wa 59 wa Kamisheni ya Idadi ya Watu na Maendeleo unaofanyika New York Nchini Marekani.
Mhe. Mchengerwa amesema Mkutano huo ambao umeanza leo Aprili 13 hadi Aprili 17 unalenga kuimarisha uhusiano kati ya idadi ya watu, teknolojia, utafiti na maendeleo endelevu, pamoja na kusaidia nchi kupanga sera bora za maendeleo kulingana na takwimu na ubunifu wa kiteknolojia.

Mheshimiwa Mchengerwa amefafanua kuwa mambo mengine muhimu yatakayoadiliwa katika vikao hivyo ni pamoja na Teknolojia katika afya ya uzazi na afya ya jamii ikiwemo teknolojia mpya za uzazi wa mpango (contraception), Utafiti katika reproductive health, matumizi ya telemedicine na digital health platforms pamoja na upatikanaji wa huduma za afya kwa vijana na wanawake.
Aidha, Mheshimiwa Mchengerwa ambaye pia ameambatana na Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia eneo la Madawa na Vifaa Tiba, Bwana Emmanauel Tayari anatarajia kutoa mada mahususi katika mkutano kuhusu Tanzania.

Pembezoni mwa vikao hivyo Mhe. Mchengerwa anatarajia kuwa na vikao kadhaa na wakuu mbalimbali wa mashirika ya Afya, na mabalozi wa nchi mbalimbali kuzungumzia masuala mbalimbali ya kimkakati katika sekta ya Afya.
Mkutano huu unahusisha zaidi ya nchi 193 kutoka sehemu mbalimbali duniani pamoja na mashiriki yote makubwa yanayojishuhulisha na masuala ya afya.


No comments:
Post a Comment