Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, Wazo Mwang'onda, amekagua na kutembelea wodi, pamoja na kuweka jiwe la msingi na kuzindua wodi ya Watoto njiti katika hospital ya Wilaya Kinondoni.
Akizungumza na wananchi, viongozi na watumishi wa Afya katika hospital ya Wilaya Kinondoni iliyopo Mabwepande, Mwang'onda amesema Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuwekeza katika sekta ya Afya kwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa ukaribu, Vifaa tiba vya kisasa na Wahudumu
Katika Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Wazo Mwang'onda, amempongeza na kumkabidhi cheti Daktari bingwa wa magonjwa ya Watoto Zena Suleiman kwa kazi kubwa anayoifanya kwa kufanya kazi ya kusaidia jamii.
Mwenge wa uhuru 2026, katika wilaya ya kinondoni, umekagua miradi 7 katika sekta mbalimbali ikiwepo maji, miundombinu ya barabara, afya, uchumi kwa vijana na Uwekezaji wa Gas, miradi ambayo imegharimu zaidi ya shilingi bilioni 9.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
No comments:
Post a Comment