HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 22, 2026

Harvard Yawakutanisha Mawaziri wa Nchi Zinazoendelea Kujifunza Uongozi

 RAIS Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho, yuko Boston, Marekani ambapo anashiriki kutoa mafunzo kwa Mawaziri wakiwemo wa Fedha na wa Mipango kutoka nchi mbalimbali zinazoendelea kupitia Mpango wa Uongozi wa Ngazi ya Mawaziri wa Harvard “Harvard Ministerial Leadership Program” inayoendeshwa na Chuo Kikuu cha Harvard.


Mheshimiwa Rais Mstaafu ni mmoja wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu wanaoshiriki kutoa mafunzo hayo.

Pamoja na Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu, wengine wanaoshiriki kutoa mafunzo hayo ni pamoja na Wakuu wa Taasisi za Kimataifa, Mashirika Binafsi na Wabobezi katika masuala ya sera, uchumi na maendeleo kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Kutoka Tanzania, mafunzo hayo yamehudhuriwa na Mhe. Khamis Mussa Omar, Waziri wa Fedha; Mhe. Prof. Kitila Alexander Mkumbo, Waziri Ofisi ya Rais - Mipango na Uwekezaji; na Mhe. Juma Malik Akil, Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad