Bi. Ngasongwa ametoa wito huo Aprili 9, 2026 wakati akifungua Mkutano wa Tatu wa Baraza la Nne la Wafanyakazi wa FCC uliofanyika Manispaa ya Morogoro.
Amesisitiza kuwa baraza hilo litumike kama jukwaa muhimu la kuimarisha mshikamano miongoni mwa watumishi na kuleta ushirikiano kati ya menejimenti na wafanyakazi katika utekelezaji wa majukumu ya taasisi.
"Baraza hili lina nafasi kubwa ya kukuza upendo na ushirikiano ili kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi zetu za kila siku." amesema Bi. Khadija
Ameongeza kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kwa mujibu wa sheria kwa lengo kushughulikia masuala ya msingi mahali pa kazi, ikiwa ni pamoja na utatuzi wa migogoro, maslahi ya watumishi na kuboresha mazingira ya kazi. Aidha, amewataka watumishi kuzingatia haki, wajibu pamoja na maadili ya Utumishi wa Umma.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Tughe Taifa Bw. Samwel Nyungwa amesema mabaraza ya wafanyakazi yameendelea kuwa kiunganishi muhimu kati ya uongozi na watumishi huku akiwapongeza FCC kwa juhudi zao katika kuboresha utendaji kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya taasisi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
FCC itaendelea kuthamini mchango wa Baraza la Wafanyakazi kama chombo muhimu cha ushirikishwaji katika maamuzi ya kimkakati na uendeshaji wa taasisi, sambamba na azma ya kujenga mazingira bora ya kazi na kutoa huduma bora kwa jamii.




Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa FCC Bi. Khadija Ngasongwa ameongoza Mkutano wa tatu wa Baraza la nne la Wafanyakazi wa FCC, uliofanyika katika Ukumbi wa Sunset Hoteli tarehe 9 - 10 Aprili, 2026 Mjini Morogoro.

















No comments:
Post a Comment