HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 28, 2026

BENKI YA EXIM YAKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutekeleza mageuzi makubwa ya elimu nchini, timu ya Benki ya Exim ikiongozwa na Afisa Mkuu wa Fedha Bw. Shani Kinswaga pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na wa kati Bw. Andrew Lyimo na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bw. Stanley Kafu ilikutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa Adolf Mkenda.

Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma, Aprili 27, 2026 kilikuwa na lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Benki ya Exim katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya elimu, zikiwemo fursa za ufadhili wa wanafunzi wa elimu ya juu hususan wanaosomea sayansi ya data (Data Science), akili unde (Artificial Intelligence) na sayansi shirikishi.

Majadiliano hayo pia yaliangazia fursa mbalimbali ikiwemo fursa za ufadhili unaoweza kutolewa na Benki hiyo, hususani kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaochukua masomo ya sayansi ya elimu ya data na akili.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad