Arusha, Aprili 1, 2026
KAMPUNI ya Airtel Tanzania imemkabidhi rasmi gari jipya aina ya Mazda CX-5 Bw. Razak, mshindi wa pili wa kampeni ya kitaifa ya “Mwaka Umenyooka na My Airtel Money App”.
Hafla ya kukabidhi zawadi hiyo imefanyika jijini Arusha, ikiwa ni hatua muhimu katika utekelezaji wa kampeni hiyo inayolenga kuwazawadia wateja na watumiaji wa Airtel Money App kote nchini.
Kampeni hiyo inawahamasisha wateja wa Airtel kutumia huduma ya My Airtel Money App kufanya miamala mbalimbali ikiwemo kutuma na kupokea fedha, kulipa bili, kununua muda wa maongezi (airtime) pamoja na kuweka fedha kwenye akaunti zao. Kila muamala unaofanywa unawaingiza moja kwa moja wateja kwenye droo ya kidijitali yenye nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali, kuanzia magari, pikipiki, TV hadi fedha taslimu.
Hadi sasa, magari mawili kati ya matatu yaliyopangwa kutolewa kupitia kampeni hiyo tayari yameshakabidhiwa. Gari la kwanza lilienda kwa Bw. Shakuu Joshua (31), dereva wa teksi kutoka Kimara–Temboni jijini Dar es Salaam. Gari la tatu bado linasubiri mshindi wake.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi hiyo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Bwa Andrew Rugamba alisema tukio hilo linaonesha dhamira ya Airtel Tanzania ya kuwazawadia wateja wake wanaotumia huduma zake mara kwa mara pamoja na kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali.
Aliongeza kuwa kampeni hiyo pia inawasaidia Watanzania kuzoea matumizi ya miamala ya kidijitali iliyo rahisi, salama na yenye ufanisi zaidi katika maisha yao ya kila siku.
“Gari la Mazda CX-5 tulilomkabidhi Bw. Mohammed Raza Roshanali leo ni zaidi ya zawadi. Ni ishara ya dhamira ya Airtel ya kuendelea kuwaletea wateja wake thamani halisi pamoja na kukuza suluhisho za kifedha za kidijitali zinazorahisisha maisha yao,” alisema ZBM huyo.
Mbali na magari, kampeni hiyo pia inatoa zawadi nyingine zikiwemo runinga janja (Smart TVs), pikipiki na fedha taslimu, hivyo kutoa nafasi kwa washiriki wengi zaidi kunufaika. Airtel Tanzania inawahimiza wateja wake kote nchini kuendelea kutumia My Airtel Money App ili kushiriki droo zilizobaki.
Kwa upande wake, Bw. Razak alisema ushindi huo utamsaidia kupunguza gharama za usafiri na kurahisisha shughuli zake za kila siku, huku pia ukitoa motisha kwa wateja wengine kushiriki kampeni hiyo.
Kupitia kampeni kama hii, Airtel Tanzania inaendelea kuonesha dhamira yake ya kuimarisha huduma zinazomlenga mteja, kuhamasisha ubunifu na kupanua matumizi ya huduma za kifedha za kidijitali nchini.

.jpeg)



No comments:
Post a Comment