Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, anatarajiwa kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa ofisi za chama hicho mkoa wa Geita. Hafla hiyo imepangwa kufanyika kesho, Machi 26, 2025.
Tukio hilo linatarajiwa kuwa na umuhimu mkubwa kwa chama hicho katika kuimarisha miundombinu ya kiutendaji katika mkoa wa Geita.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Katibu wa Siasa na Uenezi na Mafunzo wa CCM Mkoa wa Geita, Andrew Mnunke, alisema maandalizi ya hafla hiyo yamekamilika kikamilifu.
"Viongozi mbalimbali wa chama wanatarajiwa kushiriki katika hafla hii muhimu. Tunawaomba wanachama wote wa CCM kuhudhuria kwa wingi," alisema Mnunke.
Alisisitiza kuwa uwepo wa viongozi katika tukio hilo ni muhimu kama ishara ya kuunga mkono juhudi za maendeleo ya chama na kuimarisha umoja wa wanachama.




No comments:
Post a Comment