Na Mwandishi Wetu, Berlin, Ujerumani.
MKURUGENZI wa Mauzo wa Turaco Collection Tanzania, Florenso Kirambata akiziwakilisha hotel zao katika maonesho ya ITB- Berlin anasema kwamba, maonesho hayo ni eneo jema kabisa la kujitangaza kubadilishana uzoefu hasa katika dunia ambayo walaji (watumiaji wa huduma) wamekuwa wakibadilika kutokana na mazingira yanayotokea duniani.
Florenso amebainisha kuwa, Turaco Collection kwa upande wa Dar es Salaam wana Element By Westin Marriott na Delta By Marriott na kwa upande wa utalii wa kaskazini pamoja na bidhaa mbalimbali za utalii pia wana; Turaco Ngorongoro Valley Lodge Tribute portfolio under Marriott International na Turaco Manyara View Lodge Tribute portfolio under Marriott International na kwa Zanzibar wana Turaco Nungwi Beach Reasort Tribute portfolio under Marriott International na Turaco Spice Tree Stone Town Tribute portfolio under Marriott International na Beyt Aly Salaam-By Turaco
Katika jukwaa hili linalokutanisha wadau wa sekta ya utalii kutoka kila pembe ya dunia kwa lengo la kukuza ushirikiano, ubunifu na uwekezaji endelevu.
Katika hafla hii, napenda kusisitiza kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kukuza mazingira rafiki ya biashara na uwekezaji, huku ikilenga kurahisisha michakato ya kiutawala, kuimarisha mifumo ya udhibiti, na kutoa motisha zinazovutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Hatua hizi ni sehemu ya mkakati mpana wa kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utalii wa kimataifa chenye ushindani na ubora wa hali ya juu.
Tanzania imefungua milango kwa fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji, tayari ikiwakaribisha wadau kushirikiana katika maono ya kukuza uchumi endelevu na ustawi wa muda mrefu katika sekta ya utalii. Turaco Collection tunaamini kuwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali ni nguzo muhimu katika kufanikisha malengo haya.
Maonesho haya ni fursa adhimu ya kubadilishana uzoefu, kuhamasisha ushirikiano wa kimkakati, na kuweka misingi ya miradi mipya itakayoboresha miundombinu, huduma, na ubora wa uzoefu wa watalii. Kupitia jukwaa hili, tunaendelea kuitangaza Tanzania kama kivutio cha kipekee chenye utajiri wa mbuga Za wanyama,Mlima Kilimajaro,utamaduni, historia, fukwe za kuvutia na huduma bora za ukarimu.
Aidha, nawapongeza Bodi ya utalii kwa kuendeleza utamaduni wa kufanya maonesho ya utalii na uwekezaji katika medani za kimataifa.
Jitihada hizi zinaimarisha taswira ya nchi yetu, kuongeza mtiririko wa watalii, na kufungua milango mipya ya masoko duniani.
Turaco Collection tunaendelea kujizatiti kutoa huduma za viwango vya kimataifa, tukizingatia ubora, ubunifu na uzoefu wa kipekee kwa wageni wetu. Tunaamini kuwa kwa pamoja, tutaweza kuifanya Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kuwa kitovu cha utalii endelevu na wenye tija kwa kizazi cha sasa na kijacho.


.jpeg)


.jpeg)
No comments:
Post a Comment