HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 17, 2026

TTCL YALETA FURAHA KWA WATUMIAJI WA INTANETI, YAJA NA FAIBA ‘SUPERSONIC EXPERIENCE’ YENYE KASI BALAA



Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Vedastus Mwita akizungumza na vyombo vya habari katika hafla ya uzinduzi wa kifurushi kipya kijulikanano kama TTCL Faiba ‘Supersonic Experience’ Kasi Balaa. Huduma hiyo ya vifurishi inampa mteja fursa ya kupata intaneti yenye kasi, gharama nafuu pamoja na muda wa maongezi ya simu.







Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Vedastus Mwita (kulia) akifuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa kifurushi kipya kijulikanano kama TTCL Faiba ‘Supersonic Experience’ Kasi Balaa. Huduma hiyo ya vifurishi inampa mteja fursa ya kupata intaneti yenye kasi, gharama nafuu pamoja na muda wa maongezi ya simu.

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) katika hali ya kuendelea kuijenga sekta ya mawasiliano yenye nguvu zaidi na kuboresha huduma za vifurushi kwa wateja wake imekuja na kifurushi kipya kijulikanano kama TTCL Faiba ‘Supersonic Experience’ Kasi Balaa.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL, Bw. Vedastus Mwita alisema kifurushi hicho maalum chenye intaneti vyenye Kasi ya Ajabu kitamuwezesha mteJa kufanya kazi zake bila ya kuwa na wasiwasi (No Stress).

“Kama tunavyofahamu, dunia inaendelea kubadilika kwa kasi kubwa katika enzi ya hizi za  kidijitali. Leo hii, huduma za intaneti zenye kasi, ubora na uhakika zimekuwa mhimili muhimu katika kuendesha shughuli za kijamii na kiuchumi – kuanzia biashara, elimu, afya hadi ubunifu wa vijana wetu.”

“Sasa ni mwendo wa Supersonic Experience” – kasi ya ajabu, kasi isiyopimika, kwa wateja wote wa huduma ya “Faiba Mlangoni kwako”. TTCL Faiba Supersonic Experience ni vifurushi vinavyokupa nguvu ya kufanya kila kitu kidijitali bila mipaka.

“..Kuanzia Smart Home, Smart Office, gaming, streaming, biashara mtandaoni hadi mawasiliano ya uhakika, sasa yote yanawezekana kwa kasi ya ajabu kutoka TTCL,” alisema Bw. Mwita akizungumza na wanahabari.

Akifafanua zaidi juu ya vifurushi hivyo vipya, alivitaja ni pamoja na T-Fiber BUSTA chenye kasi ya 60/60 Mbps (Download and upload), Dakika 250 simu ya mezani kinachopatikana kwa Tsh 55,000 kwa mwezi, T-Fiber Triple Hub Plus chenye kasi ya 100/100 Mbps, dakika 300 simu ya mezani na GB 20 za mawasiliano ya simu ya mkononi  kinachopatikana kwa Tsh 70,000 kwa mwezi. Huku mteja akipata Simcard moja Buree.

Aliongeza vingine ni T-Fiber Triple Hub Extra – Kasi ya 150/150 Mbps, Dakika 700 simu ya mezani na GB  30 za mawasiliano - kwa Tsh 100,000 kwa mwezi. mteja akipata Simcard ya TTCL mbili, bure, T-Fiber Triple Hub Balaa – Kasi ya 200/200 Mbps, chenye dakika 1200 na GB 40 za mawasiliano - kwa Tsh 150,000 kwa mwezi. Na mteja anapata Simcard tatu buree pamoja na T-Fiber Triple Hub Jumbo – Kasi ya 250/250 Mbps, dakika 2500 na GB 50 za mawasiliano - kwa Tsh 200,000 kwa mwezi. na mteja akipata Simcard tatu za buree

Alibainisha kuwa katika mazingira haya mapya ya kidijitali, upatikanaji wa intaneti yenye kasi, gharama nafuu na uhakika si anasa tena, bali ni hitaji la msingi kwa maendeleo ya taifa; hivyo ndiyo sababu Shirika hilo limeendelea kuweka nguvu kubwa katika kuboresha miundombinu ya mawasiliano na kupanua wigo wa huduma ili kuwafikia Watanzania wengi zaidi.

“..Dira yetu ni kuona kila Mtanzania anapata fursa ya kutumia huduma ya Faiba Mlangoni Kwako itakayosaidiai kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa kidijitali – kwa kupata huduma bora, salama na za kuaminika zinazochochea maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla,”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad