HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 19, 2026

TRA DODOMA YATOA MKONO WA EID KWA WATOTO YATIMA, YAIMARISHA UPENDO NA MSHIKAMANO

 Kaimu Meneja wa Mkoa wa TRA Dodoma, Bw. Obrey Sillayo, akiambatana na Kaimu Meneja wa Huduma kwa Mlipakodi pamoja na maafisa wengine wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wametoa mkono wa Eid Fitri kwa watoto yatima na wenye mahitaji maalumu katika Kituo cha Kulelea Watoto Yatima Rahmani, ikiwa ni sehemu ya kuonesha upendo na kuimarisha mshikamano na jamii.

Akizungumza wakati wa tukio hilo, Bw. Sillayo amepongeza juhudi za kituo hicho kwa kulea watoto katika misingi bora ya maadili na malezi, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuwajali watoto hao kwa ustawi wa taifa.

Aidha, ameeleza kuwa TRA itaendelea kushiriki katika shughuli za kijamii kama sehemu ya kuwajibika kwa jamii na kujenga uhusiano mzuri na wananchi.

Kwa upande wake, Bi. Rukia Hamisi Abdallah ameishukuru TRA kwa mkono huo wa Eid, akieleza kuwa umeleta faraja na matumaini kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho.

Tukio hilo limeacha ujumbe wa upendo, mshikamano na uwajibikaji kwa jamii.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad