HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 11, 2026

TANZANIA YAELEZA MAFANIKO UWEZESHAJI UMILIKI ARDHI KWA WANAWAKE KATIKA MKUTANO WA CSW 70.

Tanzania imeeleza mafaniko iliyoyapata katika kumuwezesha Mwanamke na Mtoto wa kike kumiliki ardhi kisheria katika maeneo mbalimbali.

Akifungua Mkutano wa pembeni wakati wa Mkutano wa 70 wa Hali ya Wanawake Duniani unaoendelea jijini New York nchini Marekani, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Lucy Kabyemera amesema Tanzania imejikita katika kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi kwa Wanawake kumiliki ardhi kisheria.

Ameongeza kuwa Tanzania imekuwa ikifanya Kampeni mbalimbali za kutoa elimu kwa jamii ya umuhimu wa Mwanamke na Msichana kumiliki ardhi ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wanawake na wasichana katika umiliki wa ardhi.

Akitoa taarifa ya mafaniko hayo Mkurugenzi wa Milki, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk. Upendo Matotola amesema asilimia 28 ya wanawake nchini Tanzania wanamiliki ardhi kutokana na kuwepo kwa mazingira wezeshi hasa ya Sera ya Taifa ya Ardhi Toleo la 2023.

Amesema idadi hiyo inatarijiwa kuongezeka kwa kuwa inasimamia ulinzi na usimamizi ya Sera hiyo haki za ardhi za Mwanamke na Msichana na imendoa vikwazo vya mila na desturi hasa katika masuala ya mirathi, na inamarisha umiliki na upataji wa ardhi kwa mwanamke na msichana.

"Vile vile Mfumo wa kijidijitali wa utoaji huduma za ardhi umerahisisha utoaji wa huduma na upatikanaji wa taarifa zenye mnyumbuliko wa kijinsia ambapo mpaka sasa asilimia 34 ya wanawake wamepata huduma kupitia mfumo." amesema Dkt. Upendo

Naye Mratibu wa Kampeni ya Landa Ardhi ya Mwanamke kutoka Shirika lisilo la Kiserikali LANDESA , Khadija Mrisho amesema wataendelea kutoa elimu ya sheria juu ya haki za wanawake na kujenga uelewa wa jamii kuhusu haki za ardhi za mwanamke na msichana ili kuhakikisha jamii inaondokana na mila na desturi kandamizi hasa kwenye umiliki wa ardhi.

Aidha nchi zingine zilizoshiriki katika Mkutano huo wa pembeni kutoa mafanikio hayo ni Kenya, Uganda na Ethiopia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad