HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 23, 2026

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Kuendeleza Ushirikiano na TTCL

 

Ikulu Zanzibar | 23 Machi 2026
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Ndugu David Nchimbi, aliyeambatana na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, CPA Moremi Marwa, pamoja na ujumbe wao, waliofika kujitambulisha.

Rais Dkt. Mwinyi ameahidi kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na TTCL katika kuimarisha mawasiliano Zanzibar kupitia huduma mbalimbali zinazotolewa na Shirika hilo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL, Ndugu David Nchimbi, amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa ushirikiano unaoendelea kati ya Shirika hilo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad