HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 9, 2026

RAIS SAMIA AWAPUNGUZIA KODI WAFANYABIASHARA SOKO KUU LA KARIAKOO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa punguzo la kodi kwa wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo ambapo kwa wafanyabiashara wa vizimba wamepata punguzo la asilimia 17 huku wale wa biashara zingine kama maduka wamepata punguzo la asilimia 10 hadi 16.

Uamuzi huo wa Rais Samia umetangazwa kwa waandishi wa habari na Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo CPA. Ashraph Abdulkarim ambapo ameongeza kuwa pamoja na punguzo hilo la kodi Mhe. Rais ametoa msamaha wa kodi ya mwezi mmoja tangu alipofungua soko hilo Februari 8,2026 hadi Machi 8, 2026.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suuhu Hassan ameridhia punguzo hilo la kodi kutokana na maombi ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwake kutokana na changamoto mbalimbali walizokumbana nazo baada ya soko hili kupata ajali ya moto mwaka 2021, hivyo tunamshukuru Mhe. Rais kwa moyo wake wa usikivu na upendo mkubwa kwa wafanyabiashara” ameongeza CPA. Abdulkarim

Kabla ya kukutana na waandishi wa habari alifanya kikao na viongozi wa wafanyabiashara wa soko hilo ili kuwaeleza uamuazi wa Mhe. Rais ambapo walishukuru kwa uamuzi huo ambao umejali utu na kuwapa hamasa ya kuendelea kufanya biashara na kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa wafanyabiashara sokoni hapo, Bw. Ramadhani Kakandilo ameishukuru Serikali kwa kuwajali wafanyabiashara na kuongeza kuwa wataendelea kushirikiana na uongozi wa soko hilo ili mtaji uliowekwa na serikali uwe na manufaa kwa vizazi vya sasa na vijavyo.





No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad