HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 3, 2026

PROGRAMU YA GGML MENTORSHIP IMEWANUFAISHA WANAFUNZI WA KIKE KITAALUMA MKOANI GEITA

Geita Gold Mining Limited (GGML) imeendelea kuhamasisha ushiriki wa wasichana katika taaluma za sayansi na uhandisi kupitia programu yake ya GGML Mentorship, inayolenga kuwajengea wanafunzi wa kike ari ya kusoma kwa bidii na kujiandaa kwa fursa za ajira za baadae.

Msimamizi wa Idara ya Rasilimali Watu wa kampuni hiyo, Hadija Kisatu, amesema kuwa mara kwa mara nafasi za kazi zinazohusiana na uhandisi zinapotangazwa katika mgodi huo, wakati mwingine hakuna hata mwanamke mmoja anayejitokeza kuomba. 'Amesema hali hiyo inaweza kuathiri uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi siku zijazo, ikiwemo nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa mgodi.

“Kama wanawake hawatajitokeza kuomba kazi katika eneo la uhandisi, itakuwa vigumu siku za usoni kuwa na hata Mkurugenzi Mkuu mwanamke. Ndiyo maana tunaanza kuwajengea uwezo wasichana wakiwa bado shuleni,” amesema Kisatu.

Kwa upande wake, Mkuu wa Dawati la Jinsia wa Jeshi la Polisi Tanzania Wilaya ya Geita, Christina Katana, amewataka wanafunzi wa kike kutoa taarifa za vitendo vya ukatili bila woga ili kulinda haki na usalama wao. Amewahimiza kuripoti kwa walimu, wazazi, askari au mtu yeyote mwenye akili timamu, na kuhakikisha hatua zinachukuliwa. Aidha, amesema iwapo wataona taarifa zao hazifanyiwi kazi, wanapaswa kutafuta njia nyingine ya kufikisha malalamiko yao ili kupata msaada stahiki.


Katika kuunga mkono juhudi hizo, wahandisi wanawake kutoka GGML walitembelea Shule za Sekondari Kamena na Nyalwanzaja, ambako walizungumza na wanafunzi wa kike na kuwahamasisha kupenda masomo, kujiamini na kuwa na ndoto za kufikia malengo yao ya kitaaluma katika fani za sayansi na uhandisi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad