HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 30, 2026

NBAA YAMKARIBISHA MKURUGENZI MTENDAJI MPYA CPA PROF. SIASA MZENZI


Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imemkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa NBAA CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi  kufuatia kustaafu  rasmi kwa mujibu wa Sheria kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji CPA Pius A. Maneno ambaye amestaafu rasmi utumishi wa umma tarehe 29 Machi, 2026.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa NBAA, CPA Prof. Sylvia S. Temu akizungumza wakati wa hafla ya kumkaribisha CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi, amesema kuwa Bodi na Menejimenti nzima wanayofuraha kumpokea na kushirikiana naye kwa ajili ya kuendeleza majukumu ya Bodi katika kukuza na kusimamia Taaluma ya Uhasibu nchini.

“Leo, kwa niaba ya Bodi na Menejimenti yote ya NBAA, tunamkaribisha Mkurugenzi Mtendaji ambaye anachukua wadhifa huu baada ya kustaafu kwa Mkurugenzi wetu wa awali. Tutampa ushirikiano wa dhati na kufanya naye kazi kwa uelewa na uaminifu ili kuendeleza jukumu la Bodi la kusimamia na kukuza Taaluma ya Uhasibu,” alisema CPA Prof. Sylvia S. Temu.

Naye, CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi ameahidi kushirikiana kwa karibu na wadau wote wa Taaluma ya Uhasibu, wakiwemo Wahasibu, Wakaguzi wa Hesabu, kampuni za Ukaguzi, Serikali pamoja na washirika wa maendeleo.

“Tutashirikiana na Serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha kuwa Taaluma yetu inakua na kufikia viwango vya kimataifa, pamoja na kuimarisha uwazi na mawasiliano na wananchi kuhusu shughuli zetu,” alisema CPA Prof. Siasa Issa Mzenzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Sylvia Temu akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Siasa I. Mzenzi alipowasili katika ofisi za NBAA zilizopo jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Sylvia Temu akimkabidhi vitendea kazi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) CPA Prof. Siasa I. Mzenzi alipowasili katika ofisi za NBAA zilizopo jijini Dar Es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Prof. Sylvia S. Temu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumkaribisha Mkurugenzi Mtendaji mpya wa NBAA CPA Prof. Siasa I. Mzenzi.
Mkurugenzi Mtendaji mpya Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Siasa I. Mzenzi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokelewa katika ofisi za NBAA na Mwenyekiti wa Bodi ya NBAA, CPA Prof. Sylvia Temu pamoja na Menejimenti ya NBAA.
Menejimenti ya NBAA ikifuatilia mkutano wa waandishi wa habari mara baada ya kuwasili kwa mkurugenzi mtendani mpya wa NBAA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad