HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 19, 2026

NAIBU WAZIRI UCHUKUZI DAVID KIHENZILE ASHIRIKI MKUTANO WA KIMATAIFA WA MASUALA YA UCHUKUZI NCHINI AFRIKA KUSINI

 Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile, ameshiriki Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya Uchukuzi (NCT), mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Gallagher Estate, uliopo Johannesburg, Afrika Kusini. Mkutano huo ulifunguliwa na Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa.

Sambamba na ushiriki huo, Naibu Waziri pia ameshiriki katika Mjadala wa Mawaziri wa Uchukuzi ukiwa na Mada isemayo: “Leadership and Governance in the Implementation of an Integrated, Sustainable and Safe Transport System that Promotes Inclusive Economic Growth, Job Retention and Social Development in Southern Africa.”

Wakati wa Mjadala huo, Naibu Waziri ameeleza hatua mbalimbali zilizofikiwa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuendeleza miundombinu, ikiwemo Uwekezaji mkubwa katika Reli ya Kisasa (SGR); maboresho ya Bandari; Viwanja vya Ndege na miundombinu ya Barabara.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inaendelea kuweka mazingira rafiki ya Uwekezaji na kuwakaribisha Wawekezaji kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo ya Sekta ya Uchukuzi, kwa lengo la kuimarisha biashara; kuongeza ushindani wa kiuchumi na kukuza maendeleo ya kikanda.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad