HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 14, 2026

Meridianbet Yatoa Tabasamu la Ramadhani Kwa Msaada wa Vyakula

 


KATIKA kuuenzi mwezi mtukufu wa Ramadhani, Meridianbet imegusa maisha ya jamii kwa kutoa msaada wa vyakula na mahitaji muhimu ya nyumbani kwa familia zenye uhitaji jijini Dar es Salaam. Hatua hii imekuja kama mwanga wa matumaini kwa kaya nyingi zinazokabiliwa na changamoto, na kuwapa nafasi ya kuendelea kufunga mwezi huu wa baraka kwa utulivu.

Kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), Meridianbet imeendelea kuthibitisha kuwa mafanikio ya biashara yanaweza kwenda sambamba na ustawi wa jamii. Kampuni imejizatiti kuhakikisha kuwa msaada wake unawafikia wale wanaouhitaji zaidi, ikibadilisha changamoto za kila siku kuwa fursa ya kuleta tabasamu na matumaini mapya kwa wananchi.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, msemaji wa Meridianbet, Nancy Ingram, alisisitiza umuhimu wa kushirikiana na kusaidiana katika kipindi hiki maalum. Alieleza kuwa Ramadhani ni wakati wa kuonyesha upendo na mshikamano kwa vitendo, na kwamba Meridianbet inaamini kila msaada mdogo unaweza kuleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu.

Wananchi waliopokea msaada huo hawakusita kuonyesha shukrani zao, wakieleza kuwa msaada huo umefika wakati muafaka ambapo mahitaji ya familia huwa makubwa zaidi. Furaha na tabasamu zilionekana wazi kwa wanufaika, jambo lililodhihirisha namna msaada huo ulivyogusa maisha yao moja kwa moja.

Meridianbet imetangaza kuwa hatua hii ni sehemu ya mipango yake mikubwa ya kijamii inayolenga kusaidia sekta mbalimbali kama afya, elimu, mazingira na makundi yenye mahitaji maalum. Kupitia juhudi hizi, kampuni inaendelea kujenga daraja la matumaini na mshikamano katika jamii, hasa katika kipindi hiki cha Ramadhani.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad