HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 26, 2026

ALAF YADHAMIRIA KUENDELEA KUFANYA MAKUBWA KILI MARATHON

 



Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya ALAF Limited imeahidi kuendelea kuwekeza zaidi katika afya za wafanyakazi ikiwemo kuwekeza zaidi katika ushriki wao katika mbio za KIlimanjaro Premium Lager International Marathon ambazo zimemalizika hivi karibuni Mjini Moshi.

Meneja Rasilimali watu wa ALAF Limited Jumbe Onjero alisema hayo punde tu baada ya mgeni rasmi katika mbio hizo, Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Paul Makonda kutembelea banda la kampuni hiyo katika uwanja wa Chuo Kikiuu Cha Ushirika Moshi ambapo kampuni hiyo ilishiriki katika maonesho maalumu maarufu kama The People’s Expo yanayoandaliwa na Kilimanjaro Marathon kila mwaka.

Alisema ushiriki wa wafanyakazi katika matukio kama haya unasaidia kuimarisha afya ya mwili na akili ili kuzidisha ufanisi wao katika kazi. “Kili Marathon ni mbio kubwa sana kwa hivyo

tukaona pamoja na kuwaleta wafanyakazi kushiriki lakini na sisi kama kampuni tudhamini mbio hizi ili pia tutangaze shughuli zetu hasa ikizingatiwa tuna mpango wa kufungua show room kubwa hapa Moshi ambayo itawahudumia wateja wetu wa hapa na maeneo jirani,” alisisitiza.

Alisema walidhamini zaidi ya washiriki 50 katika mbio za mwaka huu na kwamba ushiriki wao umekuwa jambo zuri na la kukumbukwa, ambapo alisema wafanyakazi wa kampuni hiyo walishiriki katika vipengele vyote vya mbio hizo ambavyo ni kilomita 42.2 za Kilimanjaro Premium Lager, mbio za kilomita 21.1 maarufu kama YAS half marathon na mbio za kujifurahisha za kilomita 5 zinazodhaminiwa na CRDB Bank.

"Tutaendelea kuunga mkono mbio hizi kwa lengo la kuinua sekta ya michezo sambamba na kuhakikisha wafanyakazi wetu wanafanya mazoezi yatakayoimarisha afya zao kupitia mbio za Kilimanjaro International Marathon,” alisema.

Alisema mwaka jana ALAF ilizindua klabu yake ya jogging inayojumuisha wafanyakazi kutoka vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo ambapo wafanyakazi wataendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kushiriki mbio mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon pamoja na mbio nyingine.

“Tulianza kwa kushiriki tu kawaida mwaka jana lakini mwaka huu tunapoadhimisha miaka 65 tangu kuanzishwa kwa kampuni yetu tukaamua kudhamini mbio hizi kwa ukubwa zaidi,” alieleza.

Kampuni ya ALAF Limited (ALAF) ni kampuni inayoongoza kwa utengenezaji wa vifaa vya chuma vyenye ubora wa hali ya juu ambavyo ni maalum kwa ajili kuezekea paa za nyumba.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 1960, ALAF imeendelea kutoa mchango mkubwa katika sekta ya ujenzi hapa nchini.

Shughuli za ALAF hazihusiani na uzalishaji wa vifaa vya chuma za kuezekea tu bali pia ianjihusisha na uzalishaji wa koili za chuma zilionakshiwa kwa rangi kwa ajili ya matumizi mablimbali kwenye sekta ya ujenzi pamoja na mirija ya chuma na mabomba kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad