HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 19, 2026

WASHIRIKI WIZARA NA TAASISI WANOLEWA KUHUSU MFUMO WA NLMIS

Na. OWM-KAM Dodoma

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano imewapiga msasa Washiriki kutoka katika Wizara pamoja na Taasisi za Serikali kuhusu Mfumo wa Kielektroniki wa Taarifa za Soko la Ajira (NLMIS) yanayofanyika leo Februari 18, 2026 katika Jengo la OSHA, Jijini Dodoma.

Aidha, Mafunzo hayo yalilenga kuwapatia uwezo katika utoaji Taarifa za ajira wakiwa katika maeneo ya Kazi ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao ya kila Siku.

Akizungumza, Kaimu Mkurugenzi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi Bi. Alana Nchimbi katika mafunzo, amewataka washiriki kuzingatia mafunzo ya Mfumo huo ili kupata takwimu sahihi za Ajira zinazozalishwa kupitia miradi mbalimbali.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Ajira na Ukuzaji Ujuzi Bw. Godwin Mpelumbe amesema Taarifa za soko la Ajira zimetengenezwa kwa kupitia vitengo mbalimbali ikiwepo, Ukuzaji Ujuzi, Vyama vya Wafanyakazi, Sheria, Sera na Mikakati ya masuala ya soko la ajira nchini.

Kwa wakati tofauti, washiriki wa mafunzo hayo wamepongeza Serikali kwa kuanzisha mfumo huo na kuomba kutoa Elimu kwa wadau na watumiaji wa mfumo ili kuendelea kupata ujuzi na tija katika utendaji kazi wao.







No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad