HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 28, 2026

Wanawake Kupata Hati Miliki Kupitia Samia Ardhi Kliniki

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetangaza kuanza kwa kampeni maalum ijulikanayo kama “Samia Ardhi Kliniki” itakayofanyika katika mikoa yote 26 ya Tanzania Bara kuanzia tarehe 2 hadi 7 Machi 2026, kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayoadhimishwa tarehe 8 Machi 2026.Akizungumza na waandishi wa habari, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Lucy Kabyemera, amesema kliniki hiyo itaendeshwa na watumishi wanawake kutoka Ofisi za Ardhi za Mikoa yote nchini kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi.


“Kupitia Samia Ardhi Kliniki tunalenga kuwafikia wanawake wengi zaidi kwa kuwapatia elimu kuhusu haki zao za umiliki wa ardhi, kuwasaidia kitaalamu na kutoa hati miliki kwa waliokamilisha taratibu,” amesema Kabyemera.

Ameongeza kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Samia Suluhu Hassan ya kuwataka watumishi wa umma kuwafuata wananchi na kuwapatia huduma bora kwa kuzingatia utu. “Kauli mbiu ya mwaka huu ni ‘Mwanamke; Haki Yako, Miliki Ardhi Sasa,’ na tunawahimiza wanawake wote kujitokeza kutumia fursa hii muhimu,” amesisitiza.
Kwa mujibu wa Kabyemera, serikali inalenga kuongeza idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi kwani kwa sasa ni takribani asilimia 28 tu ya wanawake nchini ndio wanamiliki. “Tunaamini kumwezesha mwanamke kumiliki ardhi ni kuimarisha familia na Taifa kwa ujumla,” amesema.


 

 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad