Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Mhandisi Mussa Natty, akimuelekeza jambo Mkurugenzi wa Matengenezo ya Barabara TANROADS Mhandisi Dkt. Christina Kayoza wakati wa ziara ya ukaguzi wa barabara ya Dodoma hadi Mtera km 140.6 uliofanywa na Bodi ya Mfuko wa Barabara. Kulia ni Neema Mhondo Mjumbe wa Bodi hiyo.
**************
Na Mwandishi Wetu,Dodoma.
Hadi kufikia Februari,2026 Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS, Mkoa wa Dodoma umepokea jumla ya shilingi bilioni 15.6,kutoka Mfuko wa Barabara ambapo fedha hizo ni sehemu ya bajeti ya shilingi bilioni 18.6 zilizotengwa kwa ajili ya kazi za matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2025/26.
Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Colman Ramadhani, wakati wa ukaguzi wa barabara ya Dodoma-Mtera yenye urefu wa Km 140.6 uliofanywa na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB).
Ukaguzi huo ni sehemu ya ufuatiliaji wa kawaida wa utekelezaji wa kazi za matengenezo ya miundombinu ya barabara na tathmini ya maendeleo ya miradi ya matengenezo ya barabara inayoendelea.
Akizungumza katika ukaguzi huo, Mhandisi Ramadhani, amesema fedha zilizopokelewa zimewezesha kuendelea na utekelezaji wa kazi za matengenezo katika mtandao wa barabara unaohudumiwa na wakala huo mkoani humo.
Aidha ameeleza kuwa upokeaji wa fedha hizo umeimarisha kasi ya utekelezaji wa miradi iliyoidhinishwa chini ya bajeti ya mwaka huu wa fedha.
“Kazi za matengenezo zinaendelea katika barabara zenye jumla ya kilomita 1,707.2 pamoja na madaraja 320, ambapo mikataba 42 imesainiwa kwa ajili ya utekelezaji wa kazi mbalimbali za matengenezo," amesema Mhandisi Ramadhani.
Sanjari na hayo amesema, barabara ya Mtera-Dodoma inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo ongezeko la magari ya mizigo, hususani ya mazao na madini, ambapo yanachangia kuharakisha uchakavu wa tabaka la juu la barabara na kuongeza gharama za matengenezo.
Huku changamoto nyingine ni athari za mvua kubwa na mafuriko, hasa katika eneo la Manzase, ambapo maji upita juu ya tuta la barabara na kusababisha usitishwaji wa huduma za usafiri kwa saa tatu hadi sita kwa sababu za kiusalama.
Hata hivyo Mhandisi Ramadhani amesisitiza kuwa TANROADS Mkoa wa Dodoma itahakikisha fedha zinazotolewa na Mfuko wa Barabara kwa ajili ya kazi za matengenezo ya barabara zinatumika kwa ufanisi, ili kuboresha hali ya mtandao wa barabara mkoani humo pamoja na kuhakikisha usafiri wa barabara unakuwa salama na wa uhakika.
Zoezi la siku moja la ukaguzi wa hali ya barabara na kazi za matengenezo ya barabara ya Dodoma - Mtera limefanywa na wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Mussa Natty na Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Barabara ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mifuko ya Matengenezo ya Barabara Afrika (ARMFA), Mhandisi Rashid Kalimbaga.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara Mhandisi Mussa Natty, akifafanua jambo, wakati wa ziara ya ukaguzi wa barabara ya Dodoma hadi Mtera km 140.6 uliofanywa na Bodi ya Mfuko wa Barabara. Kushoto ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga, kushoto kwa Mwenyekiti ni Dkt. Christina Kayoza wa TANROADS na Neema Mhondo Mjumbe wa Bodi hiyo.

Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara wakipata taarifa ya athari za mvua katika eneo la Manzase kwenye Barabara ya Dodoma-Mtera km140.6, ambapo wakati wa mvua kubwa na mafuriko maji huvuka juu ya tuta la barabara na kupelekea usitishwaji kwa huduma za usafiri kwa masaa matatu hadi sita kwa sababu za kiusalama.

No comments:
Post a Comment