
Dar es Salaam, 3 Februari 2026 – Airtel Tanzania leo imekabidhi zawadi ambazo ni Tv na Bajaji kwa washindi saba kupitia kampeni yake ya miezi mitatu ya Nyoosha mwaka na myairtelapp ikithibitisha dhamira yake ya kuwazawadia wateja wanaotumia huduma za kifedha kidijitali.
Katika hafla ya
makabidhiano ya zawadi iliyofanyika leo, washindi wamekabidhiwa runinga (TV) na
bajaji zawadi zinazolenga kuboresha maisha na kufungua fursa za kwa watumiaji
wa mtandao wa Airtel. Kampeni hii inaendelea kuvutia ushiriki wa wateja kutoka
maeneo mbalimbali nchini wanaotumia Airtel Money kwa miamala ya kila siku kama
kutuma na kupokea fedha, kulipa bili na kufanya malipo kwa wafanyabiashara,
sambamba na kununua muda wa maongezi.
Tangu kuzinduliwa kwake,
kampeni ya Mwaka Umenyooka imegusa maisha ya wateja wengi kwa kutoa zaidi ya
bajaji saba, zaidi ya runinga 30, bodaboda nane, pamoja na gari moja aina ya Mazida CX5 hadi sasa. Zawadi hizi zinaonyesha dhamira thabiti ya
Airtel Money katika kuendeleza ujumuishaji wa kifedha kidijitali huku
ikiwarudishia thamani wateja wake.
Akizungumza wakati wa
hafla hiyo, Edward Mtingwa, Meneja wa Thamani kwa Wateja wa Airtel, amesema
kampeni hiyo imeundwa kuthamini uaminifu wa wateja huku ikihamasisha matumizi
ya huduma za kifedha kidijitali zilizo salama na rahisi.
“Kupitia kampeni ya Mwaka
Umenyooka, tunawapongeza na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia
Airtel Money katika miamala yao ya kila siku. Kampeni hii inaonyesha dhamira
yetu ya kurudisha thamani kwa wateja wetu huku tukihamasisha matumizi ya huduma
za kifedha kidijitali zilizo salama na rahisi,” alisema Mtingwa.
Mmoja wa washindi, Bw.
Omary Kirungi, alieleza furaha yake baada ya kupokea runinga.“Nashukuru sana
Airtel Money kwa zawadi hii. Sikutarajia kushinda, lakini sasa familia yangu
itafurahia TV mpya nyumbani. Hii imenitia moyo kuendelea kutumia Airtel Money
kwa miamala yangu ya kila siku,” alisema Kirungi.
Mshindi mwingine, Bw.
Oscar Antony, pia alitoa shukrani zake baada ya kupokea zawadi yake.“Hii ni
furaha kubwa kwangu. Zawadi hii itanisaidia sana katika maisha yangu ya kila
siku. Nawashukuru Airtel Money kwa kutambua na kuthamini wateja wao,” alisema Antony.
Airtel Money inaendelea kujizatiti kutoa suluhisho za kifedha zilizo salama, za haraka na rahisi, zinazowawezesha watu binafsi na wafanyabiashara. Kampeni ya Mwaka Umenyooka inaendelea nchi nzima, ikitoa fursa zaidi kwa wateja kushinda kila wanapofanya miamala kupitia Airtel Money.

No comments:
Post a Comment