Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Hawa Chakoma, akihitimisha mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewana OSHA kwa wajumbe wa Kamati hiyo Februari 12, 2026.
Na Mwandishi Wetu
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imesema majukumu yaWakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) yakitekelezwa ipasavyoyatalipunguzia Taifa mzigo wa kuhudumia wananchi wanaoweza kuumia au kupatamagonjwa yatokayo na kazi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Hawa Chakoma, alipokuwaakihitimisha mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHA kwawajumbe wa Kamati hiyo Februari 12, 2026.
Mafunzo hayo ya siku moja ambayo yamefanyika bungeni Jijini Dodoma ni utekelezajiwa maagizo yaliyotolewa na Kamati hiyo katika kikao cha Januari 19, 2026 OSHA ilipowasilisha taarifa kuhusu muundo na majukumu yake. Mafunzo hayo yanalengakuiwezesha Kamati hiyo kutekeleza ipasavyo jukumu lake la kuisimamia Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) na Taasisi chini yake ikiwemo OSHA.
Mheshimiwa Chakoma ameipongeza Taasisi ya OSHA kwa jitihada inazofanyakutekeleza majukumu yake ikiwemo kutoa mafunzo kwa waaajiri na wafanyakazi, kufanya ukaguzi wa mifumo ya usalama na afya ukiwemo uchunguzi wa afya za wafanyakazi katika hatua mbalimbali.
“Niendelee kuwapongeza pamoja na kuwashukuru kwa mafunzo haya ambayoyamewafungua wabunge wengi na kimsingi ni mafunzo mazuri ambayo ukiyaangaliakwa haraka haraka unaweza kudhani ni kwa ajili ya maeneo ya kazi tu lakini kiukweliunaweza kuyatumia hata katika mazingira ya nyumbani kwenye hatari tofauti tofauti,” ameeleza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii nakuongeza:
“Mafunzo haya ni kwa ajili ya kuimarisha afya za wafanyakazi na wananchi kwa ujumlana sote tunakuballiana kwamba OSHA ipo kwa ajili ya kuliokoa Taifa ambapo ikifanyakazi yake sawa sawa kwa mujibu wa utaratibu waliotueleza hapa ama hakika tutakuwatunaliokolea Taifa letu mzingo mzito wa kuwatibia wagonjwa ama kuwapa fidiawafanyakazi waliomia kazini.”
Sambamba na kuipongeza OSHA kwa kutoa mafunzo mazuri, Kamati hiyo imeitakaOSHA kuwashauri wamiliki wa sehemu za kazi kutumia teknolojia na mitambo ya kisasailiyosanifiwa katika namna inayopunguza athari nyingi za kiusalama na kiafya wakitoleamfano wa vipando (lift) zilizopo katika majengo marefu katika miji mbalimbali hapa nchini.
Aidha, Kamati hiyo imependekeza elimu ya masauala ya usalama na afya kutolewa kwawabunge wote pamoja na wanachi mbalimbali wakiwemo wakulima wadogo wadogohususan wanaojishughulisha na kilimo cha tumbaku mkoani Tabora.
“Tangu nilipoingia kwenye hii Kamati na kujua kazi zinazofanywa na OSHA natamanikuwaona kila mahali na kupitia mafunzo yetu ya leo OSHA wametoa elimu kubwa sana japo hatukuwa na muda wa kutosha,” amesema Katani Ahmad Katani, Mjumbe waKamati.
“Niwapongeze OSHA kwa mafunzo mazuri na niungane na wenzangu kusema kuwamafunzo haya ni muhimu sana na yanaweza kutusaidia sana katika maisha yetu ya kilasiku na niombe tuendelee kupatiwa mafunzo kama haya,” ameeleza Mariam Kisangiambaye ni Mjumbe wa Kamati.
OSHA ni miongoni mwa Taasisi chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusianoyenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003. Miongoni mwa majukumu ya msingi ya OSHA ni kutoamafunzo ya usalama na afya kwa waajiri, wafanyakazi na umma kwa ujumla.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano), Mhe. Deus Sanguakitoa maelezo ya awali kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii kuhusu mafunzo ya usalama na afya mahala pakazi yaliyoandaliwa na OSHA Kamati hiyo.Na Mwandishi Wetu

Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda, akitoa ufafanuzi wa masuala na hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo yaJamii baada ya mafunzo ya usalama na afya mahala pakazi,yaliyotolewa kwa Kamatihiyo Bungeni Jijini Dodoma.
Mkufunzi wa Huduma ya Kwanza Mahali pa Kazi kutoka OSHA, Bi. Moteswa Meda, akiwasilisha mada katika mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa kwaWajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Bungeni Jijini Dodoma.
Mkaguzi wa Mazingira ya Kazi na Afisa Mafunzo kutoka OSHA, Bw. Simon Lwaho, akiwasilisha mada kuhusu vihatarishi vya usalama na afya katika mafunzo ya usalamana afya mahali pa kazi yaliyotolewa kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi naMaendeleo ya Jamii Bungeni Jijini Dodoma.Mkaguzi wa Afya kutoka OSHA, Dkt. Edwin Senguo, akiwasilisha mada kuhusumagonjwa yatokanayo na kazi katika mafunzo ya usalama na afya mahali pa kaziyaliyotolewa kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii Bungeni Jijini Dodoma.

Afisa Sheria kutoka OSHA, Thomas Nsyengula, akiwasilisha mada kuhusu maudhui yaSheria Na. 5 ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi ya mwaka 2003 katika mafunzo yausalama na afya mahali pa kazi yaliyotolewa kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge yaUstawi na Maendeleo ya Jamii Bungeni Jijini Dodoma.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii,wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa katika mafunzo mafunzo ya usalama naafya mahali pa kazi yaliyotolewa na OSHA kwa Kamati hiyo Bungeni Jijini Dodoma.

No comments:
Post a Comment