HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 12, 2026

MASAUNI AMETOA RAI KWA WABUNGE KUPINGA UPOTOSHAJI KUHUSU MUUNGANO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza wakati wa semina kuhusu Muungano na Mazingira kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa jijini Dodoma, Februari 11, 2026.

*************

Na; Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni ametoa rai kwa wabunge kupinga na kusahihisha upotoshaji wa taarifa kuhusu Muungano, hususan kupitia mikutano ya hadhara na mitandao ya kijamii.

Ametoa rai hiyo wakati wa semina kuhusu Muungano na Mazingira kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa jijini Dodoma, Februari 11, 2026.

Mhandisi Masauni amesema kuwa Muungano una faida nyingi hivyo ni wakati sasa wabunge kusikiliza na kuwasilisha kwa busara hoja za wananchi kuhusu Muungano

Amesisitiza kuwa wabunge ni nguzo muhimu ya kulinda na kuimarisha Muungano wa Tanzania na wanabeba dhamana ya kihistoria ya kuhakikisha Muungano unaendelea kuwa chanzo cha amani, mshikamano na maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wa mazingira, amesema Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau imeandaa Programu ya Mageuzi ya Kukijanisha Tanzania ikiwa na lengo la kuleta mageuzi jumuishi na shirikishi yenye matokeo makubwa yanayolenga kuimarisha uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza eneo lenye uoto wa kijani kupitia upandaji miti.

Mhe Masauni amesema Julai 17, 2025 Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua Dira 2050 ambayo imetambua na kuweka nguzo mahususi ya hifadhi na ustahimivu wa mabadiliko ya tabianchi.

“Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na wadau imeandaa Programu ya Mageuzi ya Kukijanisha Tanzania ikiwa na lengo la kuleta mageuzi jumuishi na shirikishi yenye matokeo makubwa yanayolenga kuimarisha uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi kwa kuongeza eneo lenye uoto wa kijani kupitia upandaji miti.

“Kwa kuzingatia Dira 2050 imeelekeza Tanzania kuwa kinara barani Afrika katika masuala ya hifadhi na usimamizi wa mazingira, programu ambayo itawasilishwa kwa wabungeitazingatia masuala Uhifadhi wa ardhi oevu, Matumizi ya nishati safi ya kupikia, upandaji miti, biashara ya kaboni, udhibiti wa taka na usafi wa mazingira na udhibiti wa viumbe vamizi,” amesema Mhe. Masauni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira Mhe. Jackson Kiswaga amesema kupitia semina hiyo wamepata uelewa mklubwa kuhusu masuala ya mazingira.

Ameahidi kuwa pamoja na wabunge wenzao wataendelea kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi katika kuwafundisha kuhusu uhifadhi wa mazingira endelevu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni akizungumza wakati wa semina kuhusu Muungano na Mazingira kwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika katika Ukumbi wa Pius Msekwa jijini Dodoma, Februari 11, 2026.



Baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika semina kuhusu masuala ya Muungano na Uhifadhi wa Mazingira iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Dodoma, Februari 11, 2026.
Mbunge wa Viti Maalumu kundi la Wafanyakazi Mhe. Lucy Mwakyembe kutoka MkoaMjini Unguja akichangia katika semina kuhusu masuala ya Muungano na Uhifadhi wa Mazingira iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, katika Ukumbi wa Pius Msekwa Bungeni Dodoma, Februari 11, 2026.

PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad