Mwenyekiti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Seleman Kakoso Akizungunza katika ziara ya Kamati katika Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania ,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Mohamed Salum akitoa taarifa kuhusiana na TASAC wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea TASAC jijini Dar es Salaam.
Picha za matukio ya Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipotembelea TASAC jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu yatoa maagizo kwa Serikali kuweka mkakati wa kudhibiti bandari bubu kutokana kufanyika kwa biashara haramu.
Bandari bubu hizo zinatakiwa kurasimishwa na kutengenezewa miundombinu ili Serikali iweze kupata mapato.
Kamati hiyo imesema bandari bubu ni uchochoro unaotumika kupitisha bidhaa zisizohitajkika nchini
Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kutembelea Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Selemani Kakoso tayari Serikali bandari bubu ni eneo linalotumika kupitisha bidhaa haramu.
Kakoso amesema changamoto nyingine waliyobaini ndani ya TASAC ni ukosefu wa vifaa akisisitiza shirika hilo linahitaji uwekezaji mkubwa wa vifaa vya uokozi katika ukanda wa bahari, ziwa Tanganyika,Nyasa na Ziwa Victoria
“Tumeishauri Serikali kuongeza bajeti, kuweka mifumo ambayo itasaidia kupunguza ajali zinazojitokeza mara kwa mara, tumeielekeza palipo na vikwazo tuelezwe kama bunge tuchukue nafasi ya kusimamia, kazi ya bunge ni kusimamia Serikali na kuishauri pale ambapo kwao watauschukulia kama wenye maana
Kakoso amesema Tasac kuna vikwazo vya kisheria hivyo wameielekeza Serikali waharakishe mchakato kupeleka sheria bungeni kukafanyika marekebisho na sisi tupo tayari kuwasaidia ili taasisi isimame vizuri.
Aidha amesema TASAC kuendelea kuwa vifaa na mafunzo kwa wafanyakazi kutokana shughuli wanazozifanya katika kuleta ufanisi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ni Mohamed Salum amesema yapo baadhi ya maeneo ambayo hakuna miundombinu ya bandari, udhibiti wa Serikali lakini zipo shughuli zinafanyika na ndizo zinaonekana kuwa bandari bubu.
“Mwaka 2022/2023 hadi 2023/2024 tumefanya jitihada kubwa kushirikiana na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kurasimisha bandari bubu 20 katika maziwa na bahari, lakini pamoja kurasimisha bado zipo bandari bubu nyingi,”amesema.
Amesema zipo juhudi zinafanyika kuhakikisha maeneo yote yenye bandari bubu yanadhibitiwa ili kutoingizwa magendo nchini.
“Tunashirikiana na Halmashauri na maofisa uvuvi wanatoa elimu kwa wavuvi kutumia maeneo rasmi na sio kwenda kwenye bandari kavu na tutaendelea na maeneo mengine,”amesema.
Fahamu Sheria
Sheria ya Bandari Na. 17 ya mwaka 2004, kifungu cha 5, kinaipa TPA mamlaka ya kuanzisha, kuendesha na kusimamia bandari zote zilizopo Bahari ya Hindi na maziwa nchini.
Sheria hii pia inasimamia maendeleo ya miundombinu ya bandari na kuhakikisha huduma bora kwa wateja, inazuia uanzishaji wa bandari zisizo rasmi kwa kufafanua taratibu maalumu za kufuatwa kabla ya kuanzisha bandari yoyote na kuhakikisha shughuli za bandari zinasimamiwa kikamilifu na ΤΡΑ.

.jpeg)


.jpeg)

.jpeg)

No comments:
Post a Comment