Na. Josephine Majura na Peter Haule, WF, Dar es Salaam
WAZIRI wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameitaka Mamlaka hiyo kutoa elimu kuhusu Baraza hilo ili wadau wengi waweze kulitumia kutatua changamoto zao.
Mhe. Balozi Omar, ametoa maelekezo hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Baraza la Masoko ya Mitaji ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Jaji Dkt. Ntemi Kilekamajenga, katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, Jijini Dar es Salaam.
Aidha, alieleza dhamira ya Serikali ya kuendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji ili kuvutia mitaji na kukuza maendeleo ya wananchi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Masoko ya Mitaji, Mhe. Dkt. Ntemi Kilekamajenga, amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Baraza hilo ni kuwa na jukwaa maalumu kwa ajili ya usikilizwaji wa migogoro inayohusu Masoko ya Mitaji.
Alisema kuwa Baraza hilo lina Mamlaka pia ya kusikiliza migogoro inayotoka kwenye Soko la bidhaa yakiwemo masuala ya stakabadhi gharani.
Kikao hicho kimehudhuliwa pia na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Msajili wa Baraza la Masoko ya Mitaji, Dkt. Martin Kolikoli na Kaimu Kamishna Idara ya Uendelezaji Sekta ya Fedha Wizara ya Fedha Bi. Dionisia Mjema.


.jpg)
No comments:
Post a Comment