HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 25, 2026

WAZIRI KIKWETE AZINDUA JENGO JIPYA TAKUKURU CHALINZE

 





Na Khadija Kalili, CHALINZE
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Usimamizi na Utawala Bora (Mb) amewapongeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kwa kuokoa fedha kiasi cha Bil.60 zilizookolewa kwa kupitia usimamizi wa miradi mbalimbali.

Mhe Kikwete ametoa pongezi tarehe 24 Januari 2026 wakati akizundua jengo jipya la Ofisi za TAKUKURU Chalinze Mkoa wa Pwani.

Amewasisitiza TAKUKURU kutunza Jengo hilo pamoja na vifaa na samani zilizomo.

Katika hatua ingine Kikwete ametoa pongezi kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU nchini Crispin Chalamila kwamba wameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kutangaza kiasi cha fedha zilizobaki kwenye ujenzi wa Jengo hilo.

"Kwanza Mkurugenzi wa TAKUKURU acha nikupe maua yako kwa kutangaza hadharani kiasi cha fedha zilizobaki katika ujenzi Mil.8 ambazo zitatumika kwenye miradi mingine huu ni uadilifu wa gali ya juu na umethibitisha kwamba ninyi ni wazalendo na ukawe mfano kwenye Taasisi zingine za serikali nchini ambapo Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anapitisha fedha mbalimbali za miradi pale fedha zinapobaki basi zitangazwe zitafanya shughuli zingine" amesema Waziri Kikwete.

"Namshkuru Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia utawala bora nchini hivyo na sisi tunao wajibu wa kuipiga vita rushwa kwa sababu ni adui wa maendeleo yetu ,natumia jukwaa hili kukuoa maua yako kwa kazi nzuri mliyoifanya kwa taifa na kuandika historia itakayo dumu kwa taasisi hii muhimu" amesema Mhe.Kikwete.

Akizungumza kabla ya Mhe.Waziri Kikwete Mkurugenzi wa TAKUKURU Chalamila amesema kuwa bajeti ya ujenzi wa jengo hilo ilikuwa Mil.400,006 lakini hadi jengo linakamika imetumika Mi.400,006

chenji mliyoibakisha ni alama kubwa ya uzalendo na kuonesha kukiishikiapo cha utii kwamba hata kama ingebaki Shilingi kumi ungeweka wazi inaonesha kwamba wewe Chalamila ni Askari namba moja wa kupambana na adui rushwa.

Wakati huohuo amesisitiza suala la wazawa kupewa kazi katika eneo husika kwani jamii inafaidika katika mzunguko wa fedha amesema hayo kufuatia Mhandisi Hassan Matula wa Chalinze kuwa ndiye aliyesimamia ujenzi ,kwamba kwakuwa anaishi Chalinze basi kwa kupitia yeye wanachalinze wamefurahia matunda ya kazi hiyo kwa pamoja.

Aidha amesema kuwa taarifa matangazo ya miradi mbalimbali ya kazi zitangazwe kwa uwazi kwenye ubao wa matangazo kukwepa malalamiko na bila kificho.

Pia amewapongeza TAKUKURU kwa kuanzisha Klabu 132 za wapinga rushwa katika Shule za Msingi na Sekondari nchini haya ni matunda mazuri hivyo yaendelezeni na kurithisha kizazi cha vijana chuki dhidi ya rushwa .

"Kizazi kijacho cha Watanzania kinaonesha dhahiri kinachukizwa na vitendo vya rushwa ,fikirieni njia bora za kutokomeza rushwa kama viongozi na sisi watanzania tuikatae rushwa kwa vitendo.

Mkurugenzi wa TAKUKURU Crispin Chalamila amesema kuwa hadi sasa TAKUKURU wanamiliki majengo 79 na wanachangamoto ya upungufu wa majengo 66.

"Tunaahidi kulitunza jengo hili pamoja na vifaa vyake pia tunawasisitiza wananchi wakaribie kutoa taarifa za watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa" amesema Chalamila.

"Kwa sasa tumekaa eneo lenye utulivu wananchi msiwe waoga kuleta taarifa pia tunazo njia nyingi za mawasiliano kuweni huru" amesisitiza Chalamila.

Ufunguzi huo pia umehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema anawapongeza TAKUKURU kwa kufanya kazi kwa kuzingatia uwazi na uwajibikaji na kwamba mazingira ya rushwa yanazuia wawekezaji lakini kutokana na jinsi rushwa inavyodhibitiwa ndani ya Mkoa wa Pwani wawekezaji wamekuwa wakiongezeka siku baada ya siku kuja kuwekeza.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Pwani Domina Mkama viongozi wakuu kutoka Idara mbalimbali za TAKUKURU viongozi wa dini na wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad