HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 31, 2026

SG AKAGUA UJENZI WA JENGO LA OFISI MTUMBA, DODOMA

-Amuelekeza Mkandarasi akamilishe jengo kwa wakati

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali linaloendelea kujengwa kwenye mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma.

Ujenzi wa jengo hilo umefikia kiwango cha asilimia 73 na umegharimu jumla ya shilingi bilioni 16 na ili liweze kukamilika zitatumika jumla ya shilingi bilioni 26 na linajengwa kwa fedha za Serikali.

Dkt. Possi amemtaka mkandarasi, SUMA JKT na mshauri elekezi, TBA kuhakikisha kuwa jengo hilo linakamilika kwa kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa ili liweze kutumika kwa muda mrefu. Pia, amemwelekeza mkandarasi kuwa kisima cha maji ya ardhini kilichochimbwa kitunzwe ili maji yake yaweze kutumika wakati wa msimu wa kiangazi na matumizi mbali mbali ikiwemo utunzaji wa mazingira ili kuifanya Dodoma kuwa ya kijani.

“Nategemea kupata jengo lenye ubora na viwango vinavyotakiwa ili liweze kutumika kwa muda mrefu kwa lengo la kusogeza huduma karibu na wananchi na kuongeza tija na ufanisi katika mnyororo wa utoaji haki nchini,” amesisitiza Dkt. Possi.

Pia, ameongeza kuwa tunahitaji jengo liishe mapema mwaka huu ili tuhamie Dodoma kwa kuwa Ofisi hii inafanya kazi kwa karibu na Mahakama ya Tanzania ambayo tayari imehamia Dodoma.

Dkt. Possi aliambatana na Menejimeneti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, mwakilishi wa mkandarasi, Meneja Ujenzi Kanda ya Mashariki wa SUMA JKT, Kanali Saul Chiwanga na mwakilishi wa mshauri elekezi, Kaimu Meneja Miradi wa TBA, ndugu Daniel Nkruma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (wa pili kushoto) akipatiwa maelezo na mkandarasi, Meneja Ujenzi Kanda ya Mashariki wa SUMA JKT, Kanali Saul Chiwanga kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa ziara yake ya kukagua jengo hilo lililopo Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja Miradi wa TBA, ndugu Daniel Nkruma anayesimamia ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na mkandarasi, Meneja Ujenzi Kanda ya Mashariki wa SUMA JKT, Kanali Saul Chiwanga kuhusu ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali unaoendelea wakati wa ziara yake ya kukagua jengo hilo Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akiangalia ramani ya jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mkandarasi - Suma JKT na mshauri elekezi, TBA (hawapo pichani) kabla ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Asha Hayeshi akitoa maelezo mafupi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo kwa Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) alipotembelea mradi huo katika Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.
Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa Menejimenti ya Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Mkandarasi - Suma JKT na mshauri elekezi, TBA baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi hiyo unaoendelea katika Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma.




Muonekano wa jengo la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali linaloendelea kujengwa katika Mji wa Serikali, Mtumba, Dodoma

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad