HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 5, 2026

MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA AFRIKA MASHARIKI KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI NA AJIRA

-Waziri wa Nishati wa Uganda kutembelea mradi Chongolean,Tanga

Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini kutoka nchini Uganda Dkt. Ruth Nankabirwa yuko nchini kwa ziara rasmi ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bomba la kusafirisha mafura ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, ili kujionea hatua zilizodfikiwa kwa upande wa utekelezaji nchini Tanzania sambamba na mwenyeji wake Mhe. Deogratius Ndejembi.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa Habari, Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amesema, kupitia mradi wa EACOP utaleta manufaa makubwa kwenye ajira, ambapo jumla ya ajira 12,000 zimetolewa kwa vijana na wananchi wa Tanzania na Uganda wakati wa utekelezaji wa mradi huo.

Mhe. Ndejembi amesema mpaka sasa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki umefikia asilimia 79 na unatarajia kukamilika mwezi Julai mwaka 2026, huku ukichochea ukuaji wa Uchumi na ongezeko la mapato kwa nchi za Tanzania na Uganda, na kuongeza kuwa utakuwa na uwezo pia wa kusafirisha mapipa 246,000 kwa siku pindi utakapokamilika.

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini kutoka Uganda Dkt. Ruth Nankabirwa, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa nia yake ya dhati kwenye utekelezaji wa mradi huu ambao umekuwa na mafanikio makubwa na umeleta mapinduzi makubwa kwa nchi za Afrika Mashariki.

Mhe. Dkt. Ruth amesema kuwa, kuna haja ya watu wote wanaotekeleza miradi ya kimkakati kama hii wanaopatiwa ajira kuwa na utaratibu maalumu wa kuwatambua ili inapokuja miradi mingine wawe wanapewa nafasi kulingana na uzoefu na uadilifu walionao katika utendaji wa kazi huku akitolea mfano wa miradi ya gesi na umeme inayotarajiwa kutekelezwa na nchi hizi mbili .

Mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga una urefu wa kilomita 1,443 ambapo kilomita 296 ziko nchini Uganda, na kilomita 1,147 ziko nchini Tanzania ambapo kwa upande wa Tanzania kuna jumla ya vituo 4 vya kusukuma mafuta na Uganda kuna vituo 2 na kufanya jumla ya vituo vya kusukuma mafuta kuwa 6.






















No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad