HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, January 7, 2026

Kamishna wa Kamisheni ya Polisi Jamii Awasili Mkoani Mwanza leo, kwa ziara ya kikazi, Kufungua mafunzo ya siku moja kwa Maafisa wa Polisi Jamii

 


KAMISHNA wa Kamisheni ya Polisi Jamii, CP Faustine Shilogile, amewasili mkoani Mwanza leo, Januari 07, 2026, kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kufungua mafunzo ya siku moja kwa Maafisa wa Polisi Jamii kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Mafunzo hayo yatahusisha washiriki ambao ni maafisa wa Polisi Jamii kutoka Mikoa ya Mara, Tarime, Rorya, Simiyu, Geita, Tabora na Shinyanga.

Lengo kuu la mafunzo haya ni kuimarisha mikakati ya kuzuia uhalifu kabla haujatokea na endapo utatokea, usirudiwe tena, kwa mujibu wa mipango iliyowekwa na wadau husika.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza ufanisi wa Jeshi la Polisi katika kuimarisha usalama na kuendeleza ushirikiano na jamii katika kudhibiti uhalifu.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad