HaloPesa imehitimisha rasmi kampeni yake ya “Tamba na Bonasi” kwa mafanikio makubwa, baada ya kufanikiwa kuwazawadia maelfu ya wateja wake zawadi mbalimbali, ikiwemo bonasi ya hadi Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) zilizotolewa kila siku, kila wiki na kila mwezi.
Katika kilele cha kampeni hiyo, mmoja wa washindi wakubwa kutoka Zanzibar alikabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni Mbili (2,000,000). Hafla ya makabidhiano iliongozwa na Mkurugenzi wa Biashara wa Halotel Tawi la Zanzibar, Bw. Aboubakari Ngatomela, pamoja na Afisa Biashara Zanzibar, Bw. Hajjy Khamis Hajji. Tukio hilo lilishuhudiwa na wateja mbalimbali waliokuwepo katika ofisi duka la Halotel lililopo Michnzani mall, ikiwa ni ishara ya uwazi na uhalisia wa zawadi zinazotolewa kupitia kampeni ya Tamba na Bonasi.
Kupitia kampeni hii, wateja wa HaloPesa walipata fursa ya kushinda bonasi kila walipofanya miamala yao ya kila siku, ikiwemo kutuma pesa, kutoa pesa, kulipa bili na kulipia bidhaa kupitia HaloPesa. Kampeni hiyo ililenga kuhamasisha matumizi ya huduma za kifedha kidijitali, sambamba na kuwashukuru wateja kwa kuendelea kuiamini HaloPesa katika maadhimisho ya miaka 9 ya HaloPesa na miaka 10 ya Halotel.
Akizungumza kuhusu mafanikio ya kampeni hiyo, Meneja Masoko wa HaloPesa, Bi. Aidat Lwiza, alisema kuwa kampeni ya Tamba na Bonasi imekuwa chachu kubwa ya kuimarisha mahusiano kati ya HaloPesa na wateja wake kote nchini Tanzania.
“Ndani ya miaka 9 ya HaloPesa, kupitia kampeni ya Tamba na Bonasi, HaloPesa imefanikiwa kuwazawadia maelfu ya wateja wake bonasi na fedha taslimu hadi Shilingi Milioni Mbili (2,000,000). Zawadi hizi zilitolewa kila siku, kila wiki na kila mwezi kama sehemu ya kuwathamini wateja wetu wanaotumia HaloPesa katika shughuli zao za kila siku,” alisema Bi. Aidat Lwiza.
Aliongeza kuwa, HaloPesa itaendelea kuboresha huduma zake kwa makato nafuu zaidi, pamoja na kuendelea kuwaletea wateja wake ofa na promosheni mbalimbali zitakazorahisisha zaidi miamala ya kifedha nchini.
“Lengo letu ni kuendelea kurahisisha maisha ya wateja wetu kwa kutoa huduma salama, rahisi na nafuu zaidi. HaloPesa itaendelea kubuni kampeni na ofa zitakazoongeza thamani kwa wateja wetu,” alisisitiza.
Aidha, HaloPesa imewaahidi wateja wake kuendelea kuwapatia huduma bora zaidi mwaka 2026, kwa kuimarisha mifumo yake ya kidijitali, kuboresha uzoefu wa wateja na kuendelea kutoa huduma bora zitakazowafurahisha wateja wake kila siku.
Kupitia nafasi hiyo, HaloPesa imewatakia wateja wake wote Heri ya Mwaka Mpya 2026, na kuwashukuru kwa dhati kwa kuendelea kuiamini HaloPesa kama mshirika wao wa uhakika katika miamala ya kifedha.
HaloPesa inawakumbusha wateja wake kuwa mawasiliano rasmi kutoka HaloPesa na Halotel hufanyika kupitia namba 100 pekee, na inawahimiza kuendelea kutumia huduma zake ili kufurahia urahisi, usalama na thamani zaidi katika miamala yao ya kila siku.





No comments:
Post a Comment