Na Mwandishi Wetu
MWANAHARAKATI anayechochea umoja na mshikamano katika bara la Afrika, Dkt. Joshua Maponga amewaasa Waafrika kuendelea kushikamana kwa pamoja katika kulitetea na kulikomboa bara la Afrika.
Dkt. Maponga amezungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake hapa nchini Tanzania, amesema kuwa ni wajibu wa Waafrika kusimama pamoja katika kuhakikisha usawa na ukombozi wa bara lao katika nyanja mbalimbali za Uchumi, Siasa, Kijamii na hata kitamaduni.
“Nchi nyingi za Afrika zinapaswa kushikamana na kuungana kwa pamoja ili kujikomboa katika nyanja mbalimbali. Mfano Tanzania ni kama Jimbo sanjari na nchi nyingine kama Zambia, Uganda na nyinginezo, lakini nchi moja ni Afrika.
“Hivyo basi, ni lazima tuwajibike na kushikamana kwa pamoja kama majimbo ambayo yapo ndani ya nchi moja inayoitwa Afrika,” amesema Dkt. Maponga.
Aidha, Dkt. Maponga amewaasa vijana wa Afrika kuwa mstari wa mbele katika utetezi wa nchi zao. “Ni wajibu wa vijana wa Afrika kujitambua katika harakati za kulikomboa bara hili la Afrika, Vijana wanapaswa kubadilika, kufanya mageuzi na kushawishi, kuchochea maendeleo mbalimbali kwenye bara lao.


No comments:
Post a Comment