Akizungumza leo Januari 9,2026 katika kikao kazi kati ya DCEA na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari Dar es Salaam jana, Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema Tanzania imepunguza biashara haramu ya dawa za kulevya kwa kiwango kikubwa na si kama ilivyokuwa mwanzo zilipokuwa zikiuzwa hadharani na mpaka wafanyabiashara wa bidhaa hiyo kuimbwa kwenye bendi za muziki.
“Mtaani hakuna dawa za kulevya Kama heroin na Cocain pamoja dawa nyingine za kulevya na hiyo imetokana na kazi kubwa iliyofanywa na Mamlaka kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi.
“Kwa sasa huwezi kusikia tena wale waliokuwa wanaitana Zungu la Unga na wala huwezi kuona watu wakifanyabiashara ya dawa za kulevya kama tulivyokuwa tukiona huko nyuma.”
Akifafanua zaidi amesema kwa sasa Tanzania sio tena mlango la kupitisha dawa za kulevya kwani mianya yote imezibwa huku akitoa mfano zamani hata Watanzania waliokuwa wakisafiri nje ya Tanzania katika Viwanja vya ndege walikuwa wanakagakuliwa sana lakini baada ya kufanikiwa kufunga milango ya kupitisha dawa hizo hata ukaguzi umepungua.
Hata hivyo amesema baada ya kufanikiwa kudhibiti katika kupambana na dawa za kulevya hivi sasa kumeibuka tatizo lingine la ulevi wa kupindukia.
“Hivi sasa vijana wengi wameingia kwenye ulevi,baada ya kukosekana dawa za kulevya. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambanana Dawa za Kulevya tunazo Soba 78 na kwa sehemu kubwa soba hizo zimejaa Waraibu wa pombe.Hivyo tunakazi ya kupambana na ulevi.”
Kamishina Jenerali Lyimo amesisitiza kuna haja sasa hivi kuweka nguvu katika kukomesha ulevi ambao umekuwa kwa kasi kubwa sana huku akitumia nafasi hiyo kueleza umuhimu wa watu wenye uraibu kujiunga katika Soba kupata tiba.
Kuhusu kikao kazi hicho kilichowakutanisha Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini, Kamishna Lyimo amesema Mamlaka hiyo inatambua mchango wa vyombo Vya habari katika kupambana dawa za kulevya.
“Waandishi ndio suluhisho la kukomesha dawa za kulevya, hivyo tumeona iko haja ya kukutana katika kikao kazi hiki kwa ajili ya kujengana uwezo na kubadilishana uwezo kuhusu mbinu na mikakati ambayo inaweza kutufanya tuboreshe zaidi mapambana haya.

No comments:
Post a Comment