Mazungumzo hayo ni sehemu ya mwendelezo wa mikutano yake na Taasisi zilizo chini ya Ofisi hiyo, ikiwa na lengo la kufahamu utekelezaji wa majukumu yao, kusikiliza changamoto, fursa na kutoa maelekezo ya kiutendaji yatakayoongeza ufanisi, uwajibikaji na tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Katika ziara hiyo, Waziri Sangu ameambatana na Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo pamoja na mwakilishi wa Katibu Mkuu Festo Fute, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Hifadhi ya Jamii.











No comments:
Post a Comment