Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya Kampeni ya 'Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa', Bi. Flora Obeto (kushoto), akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 3 kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere (kulia), katika hafla iliyofanyika pamoja na droo ya pili ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo. Katika droo hiyo, Bw. Joseph Mafuru alishinda shs milioni 3, Bi. Xuan Lou, shs milioni 5 na Dk. Fauz Twain alijishindia shs milioni 10. Katikati ni Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Absa, Bi. Abigail Lukuvi.
Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Swere (katikati), akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya droo ya pili ya Kampeni ya 'Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa' ambapo pia mshindi wa droo iliyopita, Bi Flora Obeto (wa pili kushoto), alikabidhiwa zawadi yake ya fedha taslimu kiasi cha shs milioni 3. Katika droo hiyo, Bw. Joseph Mafuru alishinda shs milioni 3, Bi. Xuan Lou, shs milioni 5 na Dk. Fauz Twain alijishindia shs milioni 10. Kutoka kushoto ni Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Absa, Bi. Abigail Lukuvi na Mwakilishi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Neema Tatock.
Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya Kampeni ya 'Ujanja ni Kuswipe na Kadi ya Absa', Bi. Flora Obeto (katikati), akipozi kwa picha na baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania, muda mfupi baada ya kupokea mfano wa hundi ya shs milioni 3 kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Swere katika hafla ambayo pia Absa ilichezesha droo ya pili ya kampeni hiyo ambapo Bw. Joseph Mafuru alishinda shs milioni 3, Bi. Xuan Lou, shs milioni 5 na Dk. Fauz Twain alijishindia shs milioni 10.

No comments:
Post a Comment