SERIKALI imewapatia mafunzo maalum wanahabari zaidi ya 80 ikiwa ni sehemu ya mkakati na afua muhimu ya kulifanya kundi hilo muhimu ndani ya jamii kuwa mabalozi wa kukabiliana na madhara yatokanayo na usugu wa vimelea dhidi ya dawa.
Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Wizara ya Afya, Novemba 30, 2025 yameweza kuwafumbua na kuwa na uelewa mpana kwa kundi hilo muhimu ndani ya jamii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam,Desemba 30,2015 wakati wa mafunzo hayo, Mratibu wa Taifa wa Usugu wa Vimelea vya Magojwa Dhidi ya Dawa (UVIDA), kutoka Wizara ya Afya Bi. Emiliana Francis amesisitiza nafasi ya wanahabari kwenye mapambano dhidi ya UVIDA.
“Elimu na ujuzi sahihi kwenu ni chachu ya kuwa mstari wa mbele kuokoa maisha, kwani mtatoa na kuandika taarifa sahihi kwa wananchi,”amesema na kuongeza haiishii kuongeza uelewa bali pia kusaidia kupunguza vifo.
“Kwa kuwa watatumia nyenzo zao vizuri kutoa elimu kwa umma hali itakayochagiza kutumia dawa kwa usahihi na kutafuta matibabu kwa wakati.”
Kutokana na mafunzo maalum yaliyotolewa na Serikali kwa waandishi wa habari, wananchi nchini wanatarajiwa kunufaika na taarifa sahihi kuhusu matumizi ya dawa, hatua inayotarajiwa kusaidia kupunguza vifo vinavyotokana na UVIDA.
Kupitia mafunzo hayo, waandishi wa habari wamepatiwa mbinu za kuelimisha jamii kuhusu hatua muhimu zinazoweza kupunguza vifo vinavyotokana na usugu wa dawa, ikiwemo kutumia antibiotics pale tu zinapoandikwa na mtaalam wa afya.
Pia umuhimu wa kukamilisha dozi za dawa bila kusitisha kabla ya muda, kuepuka kujitibu bila ushauri wa kitaalam, kuchukua hatua za kinga zinazozuia maambukizi kutambua dalili hatarishi zinazohitaji matibabu ya haraka.
Kwa upande wao waandishi wa habari walioshiriki mafunzo hayo wameahidi kutumia majukwaa yao kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi, kwa wakati na kwa lugha inayoeleweka ili kuokoa maisha ya Watanzania.













No comments:
Post a Comment