HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 11, 2025

"VIONGOZI MUWE MABALOZI WA KAZI ZA SERIKALI" DC MOSHI

 





MKUU wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Eliakimu Mnzava, amewataka viongozi na wadau wa maendeleo kuwa mabalozi wa kuitangaza kazi inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, akisema wananchi wanapaswa kujua kiwango cha uwekezaji unaoendelea katika sekta muhimu za kijamii na kiuchumi.

Akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Mnzava amesema miradi ya miundombinu, afya, elimu, maji na umeme imeendelea kuimarika kwa kasi kutokana na fedha nyingi zinazotumwa na Serikali vijijini.

“Tumesikia hapa kwenye taarifa. Moshi imepokea fedha nyingi sana za miradi. Tusisubiri viongozi wa Serikali tu ndio tuzungumze—nendeni mkaeleze wananchi yale mnayoyaona yakifanyika.”

— Mnzava

Kikao hicho kimehudhuriwa na wabunge wa majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, viongozi wa dini, wawakilishi wa taasisi, pamoja na viongozi wa vyama vya siasa.

Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Moshi, Habibu Msangi, ameunga mkono wito wa DC, akisema ni wajibu wa kila kiongozi mzalendo kutanguliza maslahi ya Taifa kwa kutambua na kueleza kazi inayotekelezwa na Serikali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Shadrack Mhagama, amesema ofisi yake imekuwa ikitumia vyombo vya habari vya kitaifa na mikutano ya hadhara kutoa taarifa za miradi na maendeleo yanayoendelea katika wilaya hiyo.

Katika kikao hicho, taasisi mbalimbali za Serikali zilitoa taarifa za utendaji kazi na kupokea ushauri kutoka kwa wajumbe, pamoja na kueleza changamoto zinazowakabili katika utoaji wa huduma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad