Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 3,2025 Jijini Dar es Salaam.
Msama ametumia nafasi hiyo kuwaeleza Vijana kuwa wana wajibu wa kutambua amani ni nguzo muhimu katika Taifa, na kwamba wasikubali kutumika na watu wenye nia ovu na nchi yao, badala yake wanapaswa kuwa wa kwanza kuilinda amani iliyopo kwa namna yoyote
Amesema wazazi wana wajibu wa kuwakanya na kuwaonya watoto wao,kuhakikisha hawashiriki ama kukumbwa na misukumo isiyokuwa na tija.
Katika hatua nyingine, Msama amewasihi viongozi wa dini kuendelea kutoa na kuesambaza elimu ya kutetea amani na vijana kusikiliza maelekezo yao.
Msama amebainisha kuwa hata wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wanapaswa kuendelea kuhimiza vijana kuheshimu sheria za nchi, kwani hakuna haki inayoweza kutetewa nje ya misingi ya sheria na amani.


No comments:
Post a Comment