HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 5, 2025

USHIRIKIANO KATI YA FCC NA WANASHERIA NI NGUZO YA UKUAJI WA UCHUMI

Tume ya Ushindani (FCC) imeeleza kuwa katika kuelekea  Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani ni fursa muhimu ya kuimarisha ushirikiano hususan kwa wanasheria.Akizungumza katika Semina ya Kampuni za  Wanasheria juu ya umuhimu wa Sheria ya Ushindani kuelekea kwenye Kilele  cha Maadhimisho ya Siku Ushindani Duniani 2025 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Bi. Khadija Ngasongwa amesema  wanasheria ni miongoni mwa watumiaji wakubwa wa taarifa za Sheria kwa ajili ya kwenda kushauri wafanyabiashara  juu ya sheria ya ushindani.


“Wanasheria ni washauri wakuu wa wafanyabiashara na  wana wajibu wa kuhakikisha kwamba biashara zinaendeshwa kwa kuzingatia sheria, uwazi na uadilifu. Ushirikiano wao na FCC ni nguzo muhimu katika kujenga soko lenye ushindani wa haki,” alisema Ngasongwa 

Aidha, alibainisha kuwa wanasheria wanapaswa kuendelea kupata uelewa mpana wa sheria za ushindani ili waweze kuwashauri wateja wao kuhusu masuala kama upangaji bei, mikataba kandamizi na mienendo yoyote inayoweza kuathiri ushindani.

“Uchumi wa Tanzania unakua kwa kasi na ili ukuaji huo uwe imara, tunahitaji uwazi, weledi na ushirikiano wa karibu kati ya FCC na wadau wote, hasa wanasheria. Ukiukaji wa sheria za ushindani unaweza kudhoofisha uchumi, hivyo ni lazima tushirikiane kuudhibiti,” aliongeza FCC itaendelea kushirikiana katika  kulinda maslahi ya watumiaji, kuondoa vikwazo vya ushindani visivyo vya haki, pamoja na kujenga mazingira ya biashara yenye uwiano, uadilifu na ushindani unaofaa kwa wote.

Kwa pamoja, FCC na Kampuni za  wanasheria  wametakiwa kuendeleza majadiliano, kutoa elimu na kutoa ushauri unaohitajika ili kuimarisha tasnia ya  ushindani na kuwezesha wafanyabiashara kufuata sheria bila kuathiri ushindani sokoni.

Hata hivyo amesema lengo ni kuhakikisha kuwa biashara zinafanyika kwa kufuata kanuni na sheria za ushindani na hivyo utekelezaji wa sheria hiyo hauwezi kufanikiwa bila mchango wa mawakili.








No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad