HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 26, 2025

Simbachawene ataja maagizo ya Rais Samia

· Jeshi la Polisi kuwa lakutoa huduma

· Taratibu za ukamataji mtuhumiwa kurekebishwa

· Asisitiza watanzania kuipenda nchi yao

Na Mwandishi Wetu,DODOMA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameweka wazi maelekezo aliyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo yanaenda kugusa Jeshi la Polisi ambapo mabadiliko makubwa yakidhamiriwa ili kuboresha utendaji kazi wa jeshi hilo na kuweza kurejesha mahusiano mazuri na wananchi huku akiweka wazi mabadiliko hayo kuwa ni kulibadili Jeshi la Polisi kutoka matumizi ya nguvu na kuwa Jeshi la Kutoa Huduma na Urekebishaji wa Sheria katika suala la ukamataji wa watuhumiwa wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali.

Amesema hayo,wakati wa mahojiano maalumu ambapo pia ameahidi kuyafanyia kazi maoni ya Tume ya Kuangalia Jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini iliyoongozwa na Mwenyekiti Mh. Jaji Mohamed Othman Chande iliyoundwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,Januari 2023.

‘Hivi ninavyovifanya wako watu wanafikiri ninafanya mimi tu kwa matakwa yangu, Hapana ninafanya haya nimeelekezwa na Mheshimiwa Rais nifanye nini kwamba lazima uhakikishe mahusiano kati ya polisi na wananchi yanakua mazuri,kwamba wananchi wawapende polisi.Leo hii hata polisi akipata shida wananchi wanashangilia nadhani sio sawa maana polisi anatoa huduma kwa wananchi lazima tuboreshe mahusiano….’ Amesema Simbachawene

Ametaja maeneo mawili ambayo ameahidi katika kipindi chake ametumwa kuyafanyia kazi ili kupunguza na kuondoa malalamiko ya wananchi hali inayopelekea wananchi kutotii maelekezo mbalimbali ya serikali.

‘Kwanza,mabadiliko ya kimfumo, mabadiliko ya kiutashi kwa mfano mafunzo yetu ya Jeshi la Polisi lazima tuyaangalie je tunawapa mafunzo ya Kwenda kupambana na wananchi au wakawalinde wananchi,wenzetu wale wa tume ya haki jinai, iliyoundwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, wametoa mawazo mazuri sana na Rais ameagiza tuyasimamie maoni yao na mimi sasa nitakaa na Uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi,tume ya haki jinai wanasema tusiwe na Police Force bali tuwe na police service kwa kuwa ikiwa force nguvu inatumika lakini ikiwa service itakua huduma ya kipolisi ya kulinda raia na kutoa huduma na mali zao lakini nguvu sasa itakuja kwa muijbu wa sheria na kosa unalotuhumiwa nalo kulifanya lazima tukubali kuna makosa ukamataji wake lazima itumike nguvu na hilo litasemwa kwenye sheria itakayotungwa.Na pili ni ukamataji unakwenda kumkamata mtu ana kesi ndogo unatumia nguvu kubwa maana kwenye sheria kuna kesi kubwa na kesi ndogo sasa aina ya ukamataji inafanya wananchi nao wawe na pingamizi na wao watumie nguvu.’ Amesema Simbachawene

Amegusia pia suala la amani akiwaomba watanzania kuilinda nchi yao ili yasitokee kama yanayoteokea katika nchi za Burundi na Congo ambapo nchi hizo zimekosa utulivu hali inayopelekea wananchi wao kukimbia nchi zao na kuwa wakimbizi sehemu mbalimbali duniani.

‘ Hatima ya nchi ya Tanzania iko mikononi mwa watanzania, uwe una rafiki yako yuko nje ya Tanzania, uwe unampenda vipi, awe amekiusaidia vipi lakini huku Tanzania ndio wako ndugu zako, watoto wako,watanzania wenzako sasa lazima ujue kwamba ipo siku nitahitaji utulivu Tanzania na endapo amani itatoweka tukawa kama nchi za wenzetu,je wewe utakapokua umekaa peke yako moja ya majuto utakayojuta ni kama ukutoa mchango wa kurekebisha hali ikae vizuri na kumbuka katika kurekebisha vizuri sio kutia utambi ili watu waelewe unachosema.’ Amesema Simbachawene.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad