Mbunge Wambura ametoa kauli hiyo wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Geita kilichofanyika wilayani Chato, mkoani Geita. Amesema kuwa katika maeneo mengine fedha za barabara hutolewa kwa wakati na kwa kiwango kilichopangwa kwenye bajeti, hali ambayo ni tofauti na Manispaa ya Geita ambako fedha hutolewa kwa kiasi pungufu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela, amesema barabara iliyokuwa ikizungumziwa kwa muda mrefu ya kutoka Geita Manispaa kupitia Bukoli hadi Kakola, taratibu za manunuzi tayari zimekamilika, na kwa sasa taratibu za kifedha zinaendelea ili mkandarasi aanze kazi rasmi.
Naye Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Geita, Mhandisi Vedastus Maribe, amesema kwa mwaka wa fedha 2025/2026, TANROADS Mkoa wa Geita imetengewa jumla ya Shilingi bilioni 12.3 kwa ajili ya utekelezaji wa kazi za matengenezo ya barabara. Ameongeza kuwa hadi kufikia Desemba 2025, mikataba 35 yenye thamani ya Shilingi bilioni 7.4, sawa na asilimia 60.6 ya bajeti ya matengenezo, ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.





No comments:
Post a Comment