HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 12, 2025

SERIKALI YALETA NEEMA KWA WAKULIMA WA KOROSHO

 





















Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amefanya ziara ya kikazi mkoani Mtwara tarehe 11 Desemba 2025 na kutoa salamu za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa “Serikali itaendelea kuwapunguzia mzigo wakulima wa Korosho kwa kuwa na uhakika wa pembejeo za kilimo.”

Waziri Chongolo ameongeza kuwa Serikali itahakikisha Korosho zote ghafi zinazosafirishwa zitumie Bandari ya Mtwara ili manufaa na maslahi yanayohusisha mchakato wa Korosho yanaacha neema katika mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi.”

Akitoa maelekezo kwa Bodi ya Korosho Tanzania, Waziri Chongolo amesisitiza Bodi hiyo kuendelea kulinda soko la awali la Korosho ili kukabiliana na walanguzi holela (maarufu kama kangomba).

Waziri Chongolo ametembelea pia Kongani ya Viwanda iliyopo Maranje ambayo inalenga kuwa na viwanda vidogo vidogo vya kubangua Korosho ili kuwezesha wakulima kupata tija na thamani zaidi kwenye zao hilo.

Waziri Chongolo pia amesisitiza kuwa kiwanda hicho kiwe na maabara ya kisasa kupima unyevu wa Korosho ili kuhakikisha Korosho zinakuwa bora na shindanishi katika soko la Kimataifa hususan China na Vietnam.

Aidha, Waziri Chongolo amekagua Kituo cha Tafiti za Kilimo cha TARI - Naliendele, na kuwataka watafiti wake kuongeza thamani za ubora wa mbegu na kupunguza visumbufu kwa kuhuisha teknolojia na sayansi katika zao la Korosho, akitolea mfano unyunywizaji wa dawa ya viuwadudu (Sulphur) kwa kutumia teknolojia ya ndege nyuki (drone).

Pia ameitaka TARI kutambua na kuthamini mchango wa watafiti wagunduzi wa mbegu bora ili wanufaike na kazi zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad