SERIKALI ya Awamu ya Sita imesisitiza kuwa itaendelea kulea na kuwawezesha waandishi wa habari za mitandaoni na mabloga badala ya kuwashughulikia kwa mtazamo wa adhabu, ili kujenga tasnia imara na yenye tija kwa maendeleo ya taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 18 Desemba 2025, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuchukua mwelekeo wa kushirikiana na wadau wa habari badala ya kutumia hatua kali za kinidhamu.
Msigwa amesema mwelekeo huo unaendana na falsafa ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, inayojengwa juu ya ushirikiano, mazungumzo na kulinda maslahi mapana ya taifa.
Amebainisha kuwa Tanzania Bloggers Network (TBN) na Jukwaa la Mitandao Tanzania (JUMIKITA) ni wadau wakubwa wa Serikali katika tasnia ya habari, akisema mchango wao ni muhimu katika kusambaza taarifa sahihi na kuimarisha mawasiliano kati ya Serikali na wananchi.
Katika kikao kazi hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Jabiri Bakari, amesema Serikali hulazimika kuchukua hatua za kudhibiti mitandao ya kijamii kwa nyakati fulani kutokana na tofauti za sera kati ya Tanzania na wamiliki wa mitandao hiyo kimataifa, hususan pale maudhui yanapohatarisha usalama, maadili na maslahi ya taifa.
Kwa upande wake, Msigwa amewahakikishia waandishi wa habari za mitandaoni ulinzi wa Serikali, akisema endapo sheria, kanuni au sera zitabainika kuwa kikwazo katika utendaji wao, zitafanyiwa marekebisho. Pia ametangaza kuanza kwa maandalizi ya mafunzo kwa waandishi wa habari kwa kushirikiana na TCRA na kushughulikia changamoto za kodi kwa ushirikiano na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TR


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
No comments:
Post a Comment