Na Mwandishi Wetu
Serikali imesema kuwa itahakikisha wafanyabiashara wanapata mazingira wezeshi ya biashara, kupata faida, na kuchangia katika ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Patrobas Katambi alipomuwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Ushindani Duniani, yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya mwaka huu, “Akili Mnemba (AI), Walaji na Sera za Ushindani ”, inalingana na dhana ya kimataifa ya "Artificial Intelligence (AI), Consumers and Competition Policy", ikisisitiza kuwa teknolojia ya AI ni zana muhimu katika kudumisha ushindani wa haki, kulinda maslahi ya walaji, na kuongeza uwazi katika soko.
“Serikali imejipanga kuwa daraja, si ukuta, kuhakikisha sera zinazolinda walaji na wafanyabiashara zinatekelezwa ipasavyo, hususan katika matumizi ya TEHAMA na AI,” amesema Katambi na kuongeza mkazo ya mkazo katika uwekaji wa mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na walaji.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa, amesema maadhimisho yalianza kwa shughuli za kijamii, ikiwemo utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu haki zao, umuhimu wa uwazi katika masoko, na namna ya kuepuka vitendo vinavyokandamiza ushindani katika soko.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT), Jaji Rose Ebrahim, amewataka wananchi na wafanyabiashara kutoa taarifa za vitendo viovu visivyo vya haki katika soko.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani, Dkt. Aggrey Mlimuka amesema uhusiano kati ya AI na ulinzi wa walaji ni kuhakikisha uwazi na ufanisi katika biashara.
Naiibu Waziri wa Viwanda na Biashara Patrobas Katambi akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya Siku Ushindani Duniani,jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Hashil Twaib Abdallah akizungumza kuhusiana wizara itapoendelea kutoa ushirikiano kwa FCC katika kuendeleza ushindani katika soko lenye haki ,jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani FCC Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka akizungumza.
Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (FCT) Jaji Rose Ebrahim akizungumza akitoa maelezo kuhusiana namna ya utatuzi wa migogoro ya wafanyabiashara katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya ushindani Duniani yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC Khadija Ngasongwa akizungumza kuhusiana na umhimu wa maadhimisho ya Siku Ushindani Duniani katika kuendelea kusimamia ushindani katika soko kati mlaji na wafanyabiashara ,jijini Dar es Salaam.




No comments:
Post a Comment