HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 4, 2025

NEMC, UPS Waanzisha Mfumo wa kidigitali wa ufuatliaji uchafuzi wa mazingira

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesaini makubaliano ya awali na Kampuni ya United Platform Solution (UPS) kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa kidigitali wa ufuatiliaji wa uchafuzi wa mazingira katika miradi yote ya maendeleo nchini.

Hafla hiyo ya kusaini makubaliano hayo imefanyika Disemba 04,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Baraza uliopo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Bw. Dickson Mjinja ambaye pia ni Mkurugenzi wa Utawala na Fedha, amesema Baraza limefikia hatua hiyo ili kurahisisha masuala mazima ya usimamizi na uhifadhi wa mazingira kwani mfumo huo ukikamilika utarahisisha kubaini viashiria vya uchafuzi wa mazingira na kupata taarifa sahihi na kwa wakati kuhusu hali ya mazingira.

Naye Bw Mamadou Drame kutoka UPS alipozungumza amesema imekuwa azma yao kushirikiana na NEMC katika kuhakikisha uchafuzi wa Mazingira unadhibitiwa kidigitali ili kuyalinda kwa maendeleo endelevu.

Akifafanua namna mfumo huo utakavyotenda kazi, Kaimu Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji wa Sheria wa NEMC, Bw. Jamal Baruti amesema kwa sasa utaanza mradi wa majaribio ambapo vifaa maalum vitawekwa katika miradi ya mazingira ikijumuisha miradi iliyopo katika Kanda 13 za NEMC nchi nzima hali itakayoimarisha zaidi usimamizi na Uhifadhi wa mazingira nchini.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad