Mkutano huo umefanyika tarehe 8 Desemba, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa TPDC jijini Dar es Salaam, ukiwa na lengo la kujadili mikakati ya TPDC.
Pamoja na mambo mengine Mhe.Salome ameelekeza Menejimenti ya TPDC kuongeza kasi ya usambazaji wa gesi asilia majumbani na ujenzo wa vituo vya gesi asilia kwenye vyombo vya moto (CNG) ili Watanzania waendelee kunufaika zaidi na rasilimali hiyo muhimu.
Aidha, amesisitiza kuwa miradi ya utafiti na uendelezaji wa gesi asilia, ikiwemo mradi wa LNG kuanza kushika kasi baada ya majadiliano kukamilika ili kuongeza tija katika uwekezaji na kuhakikisha nchi inanufaika kikamilifu na rasilimali zake.
Katika hatua nyingine, Mhe.Naibu Waziri ameipongeza TANOIL ambayo ni kampuni tanzu ya TPDC kwa kuendelea kuwekeza kwenye biashara ya mafuta huku ikiwakilisha Kampuni ya kizawa lakini pia kuendelea kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta ya kutosha muda wote.



No comments:
Post a Comment